Saturday, January 11, 2025

MFUMO WA JUA

MFUMO WA JUA
Dhana ya Mfumo wa jua.
Ni mpangilio wa sayari nane na magimba mengine yaliyoko angani yanayolizunguka jua.
Gimba ni kitu kinachoelea angani kikilizunguka jua kupitia njia yake maalumu. Licha ya sayari nane yapo magimba mengine angani ambayo ni pamoja na vimondo, meteori, kometi, na asteroidi.
Hivyo basi, Mfumo wa jua unaundwa na jua, sayari, vimondo,meteori,kometi,asteroidi,satalaiti,vumbivumbi la angani na gesi. JUA ni gimba kubwa lenye nuru kali lililopo angani ambalo hutoa mwanga na joto na lipo katikati ya sayari zote kwenye Mfumo wake. Sayari zote nane hulizunguka jua kupitia njia yake maalumu za mzingo ziitwazo obiti.sayari hizo ni Zebaki, Zuhura, Dunia, Mirihi, Sumbula, Sarateni, Zohari, Kausi. Tofauti na magimba mengine jua halizunguki.
Published from Blogger Prime Android App

Mzunguko wa sayari kulizunguka jua
Kila sayari hujongea angani kulizunguka jua kupitia katika obiti yake.sayari hutofautiana na nyota.wakati wa usiku utaona nyota humweka na nuru yake haitulii.Nuru ya Sayari imetulia na haimweki.
Obiti au njia mzingo za sayari kulizunguka jua hutofautiana kwa ukubwa na vipenyo kutokana na umbali wa kila sayari kutoka jua lilipo na ukubwa wa kila sayari.vilevile sayari hazianguki kutokana na kani ya mvutano iliyopo kati ya Sayari hizo,nguvu hii ya uvutano ni sawa kila upande.

Asteroidi, kometi na vimondo
Asteroidi:Ni vitufe vidogo kuliko sayari vinavyoundwa kwa miamba migumu ambavyo hulizunguka jua.Asteroidi hupatikana kwenye eneo lijulikanalo kama ukanda wa Asteroidi.Eneo hili lipo katikati ya obiti ya Mirihi na obiti ya Sumbura

Kometi:Ni vitufe vidogo kuliko sayari ambavyo hulizunguka jua.Tofauti na Asteroidi,kometi zimeundwa kwa barafu zilizogandamana na vumbi la vipande vidogo vya mawe

Vimondo:Ni asteroidi na kometi ambazo hujitenga na kuja karibu zaidi na Dunia ambazo wakati wa usiku huonekana zikipita kwa kasi na zina mkia.

Aina za vimondo
(i) vimondo anga:Ni vimondo ambavyo vikiingia katika mizazi ya Dunia huungua na kuyeyuka.kutokana na hali hii watu huchanganya kati ya vimondo anga na kometi
Published from Blogger Prime Android App
(ii) vimondo nchi:Ni vimondo ambavyo vikiingia katika mizazi ya Dunia hushindwa kuungua na hivyo sehemu ngumu sana ya mabaki yake hupenya na kudondoka katika uso wa Dunia,ardhini au baharini.mfano wa vimondo hivi vilivyodondoka nchini Tanzania wilaya ya Mbozi mkoani Songwe na kingine eneo la Malampaka wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza
Published from Blogger Prime Android App
Mizazi ya Dunia ni utando mfano wa blanketi unaoifunika Dunia ili kuikinga dhidi ya vimondo na magimba mengine ya angani yasiigonge
NB:Kama kusingekuwa na mizazi ya Dunia basi kila siku dunia ingekuwa inadondokewa na vimondo na maisha yasingekuwepo Dunia I.

MIZUNGUKO YA DUNIA
Dunia inamizunguko mikuu miwili ambayo ni
     (i) Dunia kulizunguka jua
    (ii) Dunia kujizungusha katika mhimiri wake

I.DUNIA KULIZUNGUKA JUA
Dunia ni sayari ambayo binadamu huishi.dunia hulizunguka jua kwa siku 365¼ au 366.kipindi hiki cha siku 365¼ au 366 ndicho huitwa mwaka.

Mwendo wa Dunia kulizunguka jua na matokeo yake
Dunia inapolizunguka jua husababisha kutokea kwa:
(i)**Majira ya mwaka**kuna aina nne za majira ya mwaka.majira hayo ni
Published from Blogger Prime Android App
 masika(Kipindi cha mvua nyingi.kwa maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka Masika huanzia mwezi Machi hadi Mei na maeneo mengine yenye Kipindi kimoja Masika huanzia mwezi Novemba hadi Aprili),
Published from Blogger Prime Android App
Vuli(Kipindi cha mvua kiasi na jua kiasi huanzia mwezi Oktoba hadi Disemba kwa maeneo yenye vipindi viwili vya mvua),
kiangazi(majira ya mwaka yenye jua Kali,hakuna mvua kabisa pia huwa na joto kali mchana na baridi kali wakati wa usiku katika maeneo mengine) hapa Tanzania mikoa yenye Kipindi kimoja cha mvua ni sehemu ya katikati ya nchi na kusini mwa nchi kuanzia mwezi April au Mei hadi Novemba au Disemba,
Published from Blogger Prime Android App
Kipupwe(majira ya mwaka yenye baridi kali inayoweza kukausha mimea kama vile mahindi na maharage na huambatana na ukungu.katika nchi yetu ya Tanzania na baadhi ya nchi nyingi za kitropiki aina mbili za majira ya mwaka hubainika zaidi.Majira haya ni kiangazi na Masika.

(ii)**Tofauti kati ya urefu wa usiku na urefu wa mchana katika Kipindi fulani cha mwaka**Mfano Tanzania mwezi Novemba hadi Januari jua huchelewa kuzama kuliko ilivyokuwa kwa miezi ya Juni na julai.kipindi hiki Dunia huwa karibu zaidi na jua tarehe 3 Januari kila mwaka Kipindi ambacho hujulikana kama Perihelion. Mwezi Julia tarehe 6 kila mwaka Dunia huwa mbali zaidi na jua Kipindi ambacho hujulikana kama Apherion.
Published from Blogger Prime Android App

(iii)**Tofauti ya kimo cha jua la utosi kwa vipindi tofauti vya mwaka**
(iv)**kupatwa kwa jua na kupatwa kwa mwezi**Ni kuzuiliwa kwa nuru ya jua kuzifikia sayari au mwezi.sayari au mwezi huweza kuzuiliwa zisipate mwanga wa jua kabisa au huweza kuzuiliwa kiasi tu na kuacha sehemu nyingine ya Sayari au mwezi ikipata mwanga wa jua.

                 (a) **Kupatwa kwa jua**:hutokea wakati Mwezi unapokuwa katikati ya Dunia na Jua.Eneo la uso wa dunia linalofunikwa na kivuli kamili cha mwezi wakati wa kupatwa huitwa kupatwa kuliko kamili(Umbra).Aidha eneo la uso wa Dunia linalofunikwa na kivuli cha mwezi kisicho kamili wakati wa kupatwa kwa jua huitwa kupatwa kusiko kamili (Penumbra)
NB: kupatwa kwa jua hutokea wakati wa Mchana
Published from Blogger Prime Android App

               (b)**Kupatwa kwa mwezi**: hutokea wakati Dunia inapokuwa katikati ya Jua na Mwezi na kuukinga mwezi usipate mwanga kutoka kwenye jua.mwezi huweza kukingwa wote na dunia hivyo kusababisha kutokea kwa giza ghafla ambalo hudumu kwa dadika au saa kadhaa kisha nuru kurejea Tena na wakati mwingine ni sehemu tu ya mwezi hukosa mwanga wa jua na kusababisha nuru ya mwezi kufifia.
Published from Blogger Prime Android App
NB:kupatwa kwa mwezi hutokea usiku.

II.DUNIA KUJIZUNGUSHA KATIKA MHIMIRI WAKE
Mhimiri wa Dunia umekaa tenge kwa nyuzi 66½kaskazini na kusini na upande ulikoelekea haubadiliki.
Mwendo wa Dunia kujizungusha katika mhimiri wake na matokeo yake
Dunia inapojizungusha katika mhimiri wake husababisha:
Published from Blogger Prime Android App
(i)Usiku na mchana

(ii)Uvumi wa upepo
(iii)kutokea kwa mawimbi ya bahari
(iv) kuongezeka kwa kina cha bahari
(v) kutokea kwa tofauti ya muda kati ya longitude moja na nyingine
(vi)Kupwa na kujaa kwa maji

0 Comments:

Advertisement