Maana ya Internet
Ni mkusanyiko wa mitandao midogomidogo iliyounganishwa pamoja kwa Kutumia itifaki iliyokubalika dunia kote.Internet haina mmiliki au mtawala wa kati katika utekelezaji na uendeshaji wake kiteknolojia.Vilevile hauna sera ya upatikanaji na matumizi yake.Usalama wake hutegemea zaidi usalama wa mitandao janibu kuweka masharti na kanuni zake za mawasiliano.

Kuingia na kutoka kwenye mtandao
Habari zinazopatikana kwenye Internet zimehifadhiwa kwenye tovuti.Tovuti ni mkusanyiko wa wavuti.
Wavuti ni kurasa zilizoandikwa kwa lugha mbalimbali za tarakirishi.kurasa hizi kwa pamoja hujumuika katika kutoa habari au maelezo kuhusu jambo Fulani.
Ili uweze kuzifikia taarifa hizo, tarakirishi lazima iwe imewekewa Kisakuzi.Kisakuzi ni programu yenye uwezo wa kuvinjari na kutafuta habari kwenye mtandao wowote wa internet.
Katika Mfumo wa mawasiliano ya internet,kila tovuti ina anuani yake ambayo hutambulika katika internet.Anuani ya Mtandaoni huanza na herufi tatu'WWW'.Mfano ukitaka kupata habari yoyote kutoka kwenye tovuti utaandika www.msomihurutzblog.blogspot.com.Baadhi ya visakuzi vinavyojulikana ni kama'Mozilla Firefox', Microsoft Edge, Safari, Google Chrome na Internet Explorer.

Ufunguo:1=Google Chrome, 2=Microsoft Edge, 3=Safari, 4=Mozilla Firefox, 5=Internet Explorer.
Matumizi ya internet
1.Elimu: hutumika sana kwa kutafutia matini, mitihani na kupokea machapisho ya kitaaluma
2.Biashara: Internet imekuwa kiungo muhimu katika biashara. Wafanyabiashara wanatumia internet kutangaza biashara zao. Mfano huduma za kifedha kama M-pesa, Airtel money, Mixx by Yass, Halo pesa, T-Pesa
3.Afya: internet huwezesha wataalamu wa Afya kupata taarifa za kitabibu kwa kuwasiliana na wataalamu bingwa wengine.
4.Burudani: Internet imebadilisha utaratibu wa kupata burudani kwa kupakua kupitia simu yako iliyounganishwa na mtandao wa internet na kuangalia filamu.
USALAMA WA MTANDAO
Usalama wa mtandao ni muhimu kwa mtumiaji kwa kutunza taarifa zake kwa kuzingatia sera,kanuni,sheria na mipango iliyopitishwa kwa ajili ya matumizi sahihi ya internet.
Baadhi ya mambo yanayotishia usalama wa mtandao ni pamoja na:
1.Kuwepo kwa virusi wa tarakirishi
2.Kuwepo kwa wadukuzi wa mtandao
3.Kuzuia utoaji wa huduma na ucheleweshaji wa huduma
4.Uingizaji na wizi wa data
5.Wizi wa utambulisho
Mambo ya kuzingatia wakati wa kutumia internet
1.weka habari binafsi kwa uchache
2.Tunza na kumbuka nywila yako kwa usalama
3.Chukua tafadhari wakati wa kutafuta taarifa
4.Funga akaunti yako baada ya kutumia
5.Jihadhari na watu unaowasiliana nao kwenye Internet
6.Jihadhari na kile unachopakuwa
7.Jihadhari na kile unachochapisha
8.Weka programu ya usalama wa mtandao kuzuia virusi
Athari za matumizi mabaya ya internet
- Kupata maudhui yasiyofaa
- Uraibu wa matumizi ya internet
- Kufanya mawasiliano na watu waovu
- Wizi mtandaoni
- Kuvuruga mila na desturi
- Kupoteza muda
- Udanganyifu wa kitaaluma
- Kueneza virusi katika tarakirishi
- Kuvuruga amani na usalama wa nchi
0 Comments: