Friday, December 05, 2025

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                                                  OFISI YA RAIS    

                           TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAAHALMASHAURI YA MANISPAA YA TEMEKE

              MTIHANI WA UTAMILIFU KWA DARASA LA VII

SOMO : SAYANSI NA TEKNOLOJIA

MUDA SAA 1:30                                                    MWAKA        2025

MAELEKEZO

1: Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali 8,

2: Jibu maswali yote

3: Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa katika karatasi ya maswali

4: Majibu yote yaandikwe kwa kutumia Kalamu ya wino wa bluu au nyeusi

5: Onesha wazi njia itakayotumika katika kukokotoa swali pale itakapolazimika

6: Simu za mkononi haziruhusiwi katika chumba cha mtihani

7: Andika namba yako ya mtihani sehemu ya juu upande wa kulia kwenye kila kurasa

KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU

NAMBA YA SWALI

ALAMA

SAHIHI YA MTAHINI

1

 

 

2

 

 

3

 

 

4

 

 

5

 

 

6

 

 

7

 

 

8

 

 

JUMLA

 

 

SEHEMU A: ( ALAMA 10)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi kwa kuandika jibu kwenye mabano

i)       Damu imeundwa na chembechembe mbalimbali . Je ni chembechembe hai zipi husaidia mwili     kupambana na maradhi? (        )

A.   Chembe hai nyekundu,  B.  Seli hai nyeupe, C. Chembe sahani, D. Plazma, E. Seli za damu

ii)     Chembe uzi ya kike X ikiungana na chembe uzi ya kiume Y, atapatikana mtoto wa jinsia gani? (     )     A. mapacha B.Mapacha wanaofanana C. Mapacha wasiofanana D. Mtoto wa kiume E.Mtoto wa kike

iii)   Tafuta manufaa ya kimakanika  ikiwa jitihada ya 30N ilitumika kunyanyua mzigo wa 20N.

A.   2  B. 4 C.3, D. 6 , E. 10.       (            )

(iv)Ni ugonjwa upi kati ya magonjwa yafuatayo huathiri zaidi wanaume?

      A. Anemia Selinundu,  B. Hemofilia, C. Uzeruzeru, (              )

     D. HIV/AIDS E. Pepopunda.

(v)     Kipindi ambacho mwanamke anakosa hedhi kutokana na umri kinaitwa:-

(        )

    A.Kubalehe, B. Kukoma hedhi, C. utasa, D. Kujitambua, E. Ukeketaji.

( v) Chunguza kielelezo kifuatacho kisha jibu swali;

(vi)   Mchoro hapo juu ni nyenzo daraja la ngapi?

       (           )

A. Nyenzo daraja la kwanza, B. Nyenzo daraja la pili. C. Nyenzo daraja la tatu,

D. Nyenzo daraja la nne,    E. Nyenzo daraja la tano,

(Vii)Mionzi ya jua hufika katika uso wa dunia kwa njia ya :

                A. Mpitisho B. Mnuururisho C. Kuvukiza  D. Msafara E. Difyusheni              (           )

Viii) Ipi kati ya zifuatazo huonesha muunganiko sahihi kati ya oksijeni na haidrojeni?

                  A.HcL,  B. H2  C. H2O,  D. Co2 E. OH.       (           )

(ix) Kokotoa รผkinzani katika jiko la umeme ikiwa mkondo wa umeme ni 6A, na tofauti ya  potenshali ni 120V.

                   A. 4 ohms  B. 3 ohms C. 20hms  D. 0.2 ohms  E.200hm                   (           )

(x)Kuna aina nyingi za udongo. Udongo unaofaa  zaidi kwa kilimo ni

  A. Udongo wa kichanga,  B. Udongo tifutifu, C. Udongo wa Mfinyanzi,

                  D. Mbolea,  E. Udongo  wa kichanga na mfinyanzi            (           )

2.   Oanisha dhana za kisanyasi kutoka orodha A na maana  zake kutoka orodha B. kwa kuandika herufi ya jibu sahihi katika nafasi ya jibu iliyotengwa

Na

Orodha A

 

Orodha B

i

Alama ya umeme inayowakilisha umeme wenye mkondo mkubwa

 

A

ii

Mimea hufyonza maji kupitia mizizi kwa njia ya

 

A.Osmosis B.Transpiration C.Uchavushaji

D. Difyusheni E. Fotosinthesis.

iii

Mkusanyiko wa  mkeka kazi mmoja au zaidi huitwa

 

A. Data B. Kitabu kazi  C. Programu D. Torakishi E. Seli

iv  

      

      

      

    Daraja la moto linalosababishwa na    kuungua kwa gesi zinazowaka kama    vile butani, propani, methani na    asetilin

 

A. Daraja A,  B. Daraja  B, C. Daraja C,  D. Daraja F

v

Hewa ni mkusanyiko wa gesi mbalimbali. Je, gesi inayowezesha vitu kuwaka ni

 

A. Oksijeni  B. Kabonidayoksaidi. C. Nitrojeni  D. Argoni

E. Haidrojeni.

3.   Kamilisha sentensi kwa kuandika jibu sahihi kutokana na maelezo ya swali yaliyotolewa

(i)        Jotoridi la mwili wa ndege ni 40°C. Badili  jotoridi hilo kuwa Fahareinheit (0F).....................

(ii)     Umeng'enyaji wa chakula huanzia mdomoni hadi kwenye utumbo mwembamba, Chakula

ambacho humengenywa mdomoni (kinywani) ni ..........................................................................

(iii)   Njia ya asili mawasiliano iliyotumika na watu mbalimbali ni................................................

(vi) Fuatilia mlishano ufuatao

      SIMBA               SWALA                 MAJANI.     Nini kitatokea  endapo Simba atatoweka?

(v) Moja kati ya tabia za viumbe hai ni kutoa Uchafu. Taja viungo ambavyo vinahusika  na utoaji wa taka mwili : .............................................................................................................

SEHEMU B:  ( Alama 20 )

4. Jaza nafasi, zilizoachwa wazi katika swali la 4-6. kwa kueleza kwa ufupi

4)i) Wanafunzi wa darasa la tano walichuma  jani la mmea (kijani) na kulitia katika kimiminiko      fulani, Matokeo yake jani lilibadilika rangi kuwa nyeusi . Kimiminika kilichotumika ni

.......................................................................................................................................................

ii) Jiwe lina uzito wa 100N likiwa hewani ikiwa  kanielezi ndani ya kimiminika ni 20N.Tafuta uzito wa jiwe likiwa ndani ya kimiminika ....................................................................................

5 i)  Mwalimu Anna alitumia kifaa fulani kuingiza alama za somo la hisabati katika tarakilishi .

Taja jina la kifaa alichotumia kuingizia alama ..............................................................................

(ii) Mwajuma amejifungua mtoto leo, Chakula cha asili cha mtoto wake mchanga ni

........................................................................................................................................................ 5iii)  Bahati alifunika mshumaa kwa hutumia glasi Baada ya muda mshumaa ukazimika. Nini

kilisababisha mshumaa kuzimika?....................................................................................................

6i)Hewa  ni  mchanganyiko wa gesi mbalimbali kama vile oksijeni kabonidayosaidi na nitrogeni .

Je kabonidayoksaidi inachukua asilimia ngapi ya gesi zote ?............................................................

ii)    Chunguza mchoro ufuatao kisha tambua herufi inayowakilisha kuyeyuka kwa maada:

........................................................................

iii)  ASIDI + BASI = CHUMVI + MAJI . Je, mpambano huu wa kikemikali huitwa........................

  SEHEMU  C ( Alama 10)

Chunguza picha, michoro na kokotoa kwa huonesha  njia kujibu maswali yafuatayo:

7.(i)Densiti ya kitu ni  kg 80m³ Ikiwa tungamo la kitu ni kg 240, Tafuta ujazo. wa kitu hicho.

(ii) Kwa nini baiskeli ni mashine tata?

iii) Ikiwa gesi ya haidrojeni itaungana na gesi ya okisijeni nini kitatokea?

8 i) kani   inayosababishavitu kuelea huitwa............................................................................

(ii) Kifaa ambacho hunasa na kusambaza mawimbi Sumaku  umeme katika vifaa kama redio,

    simu na runinga huitwa ..............................................................................................................

 

 

Imeandaliwa na:

                             Nampunguprimary2@gmail.com

 

Msomihuru blog is an educational blog that provides clear, insightful, and practical knowledge on academics, society, technology, literature, science, and personal development. Learn freely, grow daily.

0 Comments: