KISA CHA MKULIMA NA KUKU ALIYETAGA MAYAI YA DHAHABU .
Leo hatujapata makala ya asubuhi kutokana na sababu na sababu fulani hivyo tukumbushie hii nikiwa naendelea kuandaa makala ya "CHUO KIKUU NI KIWANDA". Ni makala itakayowalenga zaidi wanachuo, waliohitimu na wanaotarajia kwenda chuo.
Kulikuwa na mkulima mmoja kwenye Kijiji kidogo kilichokuwa kinakaliwa na watu wa hali ya chini. Mkulima huyu alikuwa ni mcha Mungu na mwenye utu sana. Mkulima huyu alikuwa na mke na watoto watatu. Waliishi maisha yao duni huku wakilima kwa msimu na walijishughulisha na ufungaji wa kuku. Hali ya umasikini iliwakosesha furaha na kila siku walimuomba Mungu walau awashushie neema ya kutajirika. Mkulima huyu aliamini ipo siku kuna neema itawafikia maisha yao yatabadilika .
Siku moja mkulima aliingia kwenye banda la kuku ili akusanye mayai na alishangaa kuona kuku wake ametaga yai la tofauti. Yai lilikuwa liking'aa tofauti na mayai mengine. Moyo wake ulijawa na hisia za furaha. Alilibeba na kukimbia kumuonyesha mkewe. Wote wakaambiana kuwa mbona kama yai ni madini ? Wakakubaliana mume aende kwa wataalamu wa madini. Alipofika akaambiwa ni Dhahabu. Basi akaiuza pale na kupata fedha nyingi. Hapo akanunua zawadi kama nguo za watoto wao, za mkewe na yeye pia. Alinunua mahitaji mengi. Akarudi nyumbani.
Mke na watoto wao walifurahi sana, wakanunua Tv kubwa ya kisasa na redio. Baada ya siku kadhaa yule kuku alitaga yai jingine la Dhahabu. Kama kawaida wakaenda kuliuza. Mkulima akajenga nyumba kubwa mpya. Familia hii ikaona neema ya ajabu maishani. Wakanunua magari ya mume na mke. Wakawa ni watu wa tofauti sana pale kijijini. Kila mtu aliwashangaa na kutamani maisha yao. Wengine walikwenda kuomba vibarua na walipewa. Pesa ipo sema kingine.
Kuku aliendelea kutaga yai la dhahabu kila baada ya siku kadhaa, na walipopata walifanya matumizi yao makubwa. Walibadili mtindo wa maisha. Wakawa wanakwenda kuvinjari maeneo ya kifahari hoteli za nyota tano. Waliajiri walinzi walinde nyumba yao na usalama wao. Watoto wao wakapelekwa shule za kulipia tena ni Intaneshino.
Kwa kuwa kuku wao aliwapa uhakika wa maisha,ukawa wakitumia zikaisha wanakopa na kulipa kuku akitaga yai na kuliuza. Mwanamke alipendeza na kurudi kwenye ubinti. Unajua tena shida ya umasikini unakufubaisha utadhani mfanyakazi wa kiwanda cha sementi . Yaani umri wa kijana unaonekana kibabu nyie. Mkulima akawa msela akatafuta na nyumba ndogo. Unajua ukitajirika unapendwa hata kama umri umekwenda utaitwa mzee kijana.
Ikafika siku kuku hakutaga yai. Mkulima akahamaki sana. Ikabidi amuite mtaalamu wa kuku wakampa dawa lakini bado hakuonesha dalili za kutaga. Mkulima na mkewe wakawaza sana juu ya tatizo la kuku wao. Baada ya siku za kusubiri matatizo yakawaandama, madeni yakaanza kuwasumbua. Wakakata shauri la kumchinja kuku ili wampasue tumboni watoe mayai yote kwanza kwa kutaga moja moja alikuwa anawachelewesha. Mfa maji haishi kutapa tapa.
Mkulima na mkewe walipigwa butwaa baada ya kumpasua kuku na kukuta hata kipande cha yai hakuna. Mkulima akazirai kwa muda na mkewe akampa huduma ya kwanza. Waliingia kikao cha dharura huku wakilaani kuku wao. Walianza kuuza magari na vingine ili walipe madeni. Hali ya maisha yao ikaanza kuzorota. Outing na shopping za maana zikakata. Nywele za gharama kwa mke hazikusukwa tena.
Baada ya miaka mitano, mkulima yule alikuwa ameshafilisika na hata kushindwa kuendelea kuwalipia watoto wake ada. Marafiki na machawa wake hawakuonekana tena. Alishikwa na msongo wa mawazo. Magonjwa nyemelezi yakaanza. Akaugua na fedha za matibabu zikakosa. Akatibiwa kinyonge akafa. Watoto walilia sana. Mke akalia sana. Baada ya miaka miwili mke nae akafariki kwa shinikizo la moyo. Makaburi mawili yakawa burudani ya macho ya watoto wao. Jamii iliwadhihaki sana kuwa walikuwa wanaringa kusoma shule za hadhi kubwa, sasa Kiko wapi? Wao na D mbili wanapeta.
Funzo.
1. Mkulima ni wewe mwajiriwa kuku ni ajira yako anayekutagia mshahara. Yai la dhahabu usilile liache lianguliwe upate kuku wengi zaidi watakao Taga mayai ya Dhahabu uuze uwe Milionea. Kumbuka kuweka akiba kila mshahara na Fanya Uwekezaji bila kuacha.
2. Mkulima ni wewe uliyejiajiri ukidhani uko salama. Umeanzisha biashara inakutegemea kila kitu, usipokuwepo na yenyewe haipo. Kuku ni biashara na Mauzo ni yai la dhahabu. Tenga kiasi cha faida weka Akiba na Fanya Uwekezaji ambao haukutegemei wewe moja kwa Moja kufanya kazi.
3. Mkulima ni wewe msanii wa muziki au mtumia kipaji. Kipawa chako ni kuku na Dhahabu ni malipo ya Kazi zako. Wekeza.
4. Hata nyie wakulima kwanini hivi nani aliyewaroga? Yaani unauza mazao yako shambani? Unalima kwa shida, unapigwa mvua na jua wewe na mkeo, mbolea ghari lakini ukivuna unahamia mjini kwenda kuponda mali kufa kwaja. Unakuwa busy kulisha vibinti vya baa. Ama kweli teseka Malaya ale. Unajua ukiwa masikini akili zinaondoka Kichwani.
5. Masikini akipata matako hulia mbwata. Unajua kitu cha Msingi hapa najifunza kwa Suleimani yule tajiri wa kwenye Biblia aliyemiliki wake 700 na michepuko 300 na bado zikaiva na Mungu. Sasa kabla hajatoboa Mungu alimuuliza nikupe nini? Jamaa akasema Hekima na maarifa. Unajua wakush tunakosea sana unamuomba Mungu akupe mali halafu akili huna, anakubariki halafu zinakuua.
6. Chunga sana tabia zako unapokuwa umepata. Unajua kuna watu wanaonekana wema kabla hawajafanikiwa ila akizipata ndo utajua nyani huonwa makalio kipindi anakwenda juu ya
Imeandaliwa na :Mwl Ibrahim Jumanne 0743080401
0 Comments: