Sunday, June 14, 2026

Jinsi ya Kuhesabu Tofauti ya Muda Duniani kwa Kutumia Longitudo | Geography Notes

Jinsi ya Kuhesabu Tofauti ya Muda Duniani kwa Kutumia Longitudo | Geography Notes

Lengo: Mwanafunzi aweze kuhesabu muda wa sehemu moja ya dunia kwa kutumia longitudo.



Hatua ya 1: Tambua Longitudo za Sehemu Husika

Mfano:
Tanzania = 45° Mashariki
Marekani = 75° Magharibi

Hatua ya 2: Tafuta Tofauti ya Longitudo

Kama ziko pande tofauti za Greenwich (Mashariki na Magharibi), jumlisha:

Kama ziko upande mmoja, toa ndogo kutoka kubwa.

Hatua ya 3: Badilisha Longitudo kuwa Saa

Kumbuka:
15° = Saa 1
1° = Dakika 4
Mfano:

Hatua ya 4: Tambua Nani Yuko Mbele kwa Muda

Mashariki = mbele kwa muda
Magharibi = nyuma kwa muda
Kwa hiyo Tanzania (Mashariki) iko mbele ya Marekani (Magharibi) kwa saa 8.
Hatua ya 5: Ongeza au Punguza Saa
Ikiwa Tanzania ni saa 2:00 usiku:
Marekani iko nyuma kwa saa 8
2:00 − 8 = 18:00 (saa 12 jioni)

Maswali ya Mazoezi

1.Tanzania (45°E) ni saa 10:00 jioni. Je, nchi iliyopo 15°E ni saa ngapi?
2.Tanzania (45°E) ni saa 6:00 mchana. Je, nchi iliyopo 75°E ni saa ngapi?
3.Tanzania (45°E) ni saa 4:00 asubuhi. Je, nchi iliyopo 30°W ni saa ngapi?

Kanuni ya kukumbuka:

Mashariki huongeza muda, Magharibi hupunguza muda.

0 Comments: