Saturday, July 25, 2026

Jinsi ya Kujisajili kama Private Candidate NECTA Form Six 2027/2028

 Fahamu Jinsi Ya Kujisajili Kama Private Candidate Kufanya Mtihani Wa Necta Form Six

Watu wote wanaotarajia kufanya Mtihaniwa Kidato cha Sita (ACSEE) kama Watahiniwa wa Kujitegemea;

1. Kipindi cha usajili kwa Watahiniwa wa Kujitegemea huanza mwezi wa 7 na huisha mwezi wa 9. Ada ya usajili ni Shilingi 50,000/=, watakaojisajili kwa kuchelewa yaanikuanzia tarehe mwezi wa 10 watalipa Shilingi 65,000/= ikiwa ni ada yakawaida pamoja na faini.

2. Kabla ya kusajiliwa na Mkuu wa Kituo kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye Vituo vya Mitihani kuchukua namba rejea (reference numbers) zinazotolewabure na kufanya malipo ya ada kupitia Benki kwa kutumia ‘Control Number’.

3. Ufafanuzi kuhusu utaratibu wa hatua za kufuata katika kutengeneza ‘Control Number’na kujisajili, umetolewa katika tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania: https://www.necta.go.tz/news/read/73


4. Waombaji wote wasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwani mfumo wa usajiliutafungwa mara baada ya kipindi cha usajili kukamilika.

Testme ni mwalimu wa shule ya Awali na Msingi na mwandishi wa maudhui ya elimu nchini Tanzania. Kupitia blog ya MsomiHuru Na Mitihani Tz, anashiriki mitihani, vitabu, andalio la somo, na nyenzo mbalimbali za kujifunzia kwa wanafunzi na walimu.

0 Comments: