PROGRAMU YA PAINT – SAYANSI DARASA LA NNE
1. Maana ya Programu ya Paint
Paint ni programu ya kompyuta inayotumika kuchora, kupaka rangi, kuandika na kufanya marekebisho rahisi kwenye picha. Ni mojawapo ya programu zinazoweza kutumiwa na wanafunzi kujifunza kwa kutumia michoro.
2. Matumizi ya Programu ya Paint
Programu ya Paint inaweza kutumika kwa:
- Kuchora picha mbalimbali.
- Kupaka rangi kwenye michoro.
- Kuchora maumbo kama duara, mraba na pembetatu.
- Kuandika maneno kwenye picha.
- Kufuta sehemu ya mchoro.
- Kubadilisha au kurekebisha picha.
- Kutengeneza michoro ya kuelezea masomo ya Sayansi.
- Kuhifadhi picha iliyochorwa.
3. Vifaa Muhimu vya Paint
A. Pencil
Hutumika kuchora mistari midogo au michoro kwa mkono.
B. Brush
Hutumika kuchora kwa kutumia mistari yenye unene mbalimbali.
C. Eraser
Hutumika kufuta sehemu isiyohitajika kwenye mchoro.
D. Fill with Color
Hutumika kujaza eneo fulani la mchoro kwa rangi.
E. Shapes
Hutumika kuchora maumbo mbalimbali kama:
Mduara
Mraba
Mstatili
Pembetatu
Mstari
F. Text Tool
Hutumika kuandika maneno kwenye mchoro.
G. Colour Palette
Hutumika kuchagua rangi zinazotumika kwenye mchoro.
H. Select
Hutumika kuchagua sehemu fulani ya picha ili kuisogeza, kuinakili au kuifanyia marekebisho.
4. Jinsi ya Kufungua Paint
Hatua za kufungua Paint kwenye kompyuta:
1.Washa kompyuta.
2.Bonyeza Start.
3.Tafuta programu ya Paint.
4.Bonyeza Paint.
5.Ukurasa wa kuchorea utafunguka.
5. Jinsi ya Kuchora kwa Paint
1.Fungua programu ya Paint.
2.Chagua Pencil au Brush.
3.Chagua rangi unayotaka.
4.Tumia mouse kuchora kwenye eneo la kuchorea.
5.Tumia Eraser kufuta makosa.
6.Tumia Shapes kuchora maumbo.
7.Tumia Fill with Color kupaka rangi.
8.Hifadhi kazi yako.
6. Jinsi ya Kuhifadhi Kazi
Baada ya kumaliza kuchora:
1.Bonyeza File.
2.Chagua Save As.
3.Chagua mahali pa kuhifadhi.
4.Andika jina la picha.
5.Bonyeza Save.
7. Matumizi ya Paint katika Sayansi
Paint inaweza kusaidia mwanafunzi kuchora na kuelezea vitu vya Sayansi, kwa mfano:
1.Sehemu za mmea.
2.Sehemu za mwili wa binadamu.
3.Wanyama.
4.Mzunguko wa maji.
4.Mfumo wa Jua.
5.Vifaa vya maabara.
6.Mazingira.
7.Vyanzo vya maji.
Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kuchora mmea, kuweka rangi mbalimbali na kuandika majina ya sehemu zake kama mizizi, shina, majani na ua.
8. Faida za Kujifunza Paint
Huongeza ubunifu wa mwanafunzi.
Husaidia mwanafunzi kuelewa kwa kutumia picha.
1.Hukuza ujuzi wa kutumia kompyuta.
2.Husaidia katika kuchora michoro ya masomo.
3.Humwezesha mwanafunzi kujifunza kuchagua na kutumia rangi.
4.Husaidia mwanafunzi kufanya kazi kwa umakini.
9. Tahadhari Wakati wa Kutumia Kompyuta
Mwanafunzi anatakiwa:
1.Kutumia kompyuta kwa uangalifu.
2.Kutogusa nyaya bila ruhusa ya mwalimu.
3.Kutokula au kunywa karibu na kompyuta.
4.Kutumia mouse na keyboard kwa usahihi.
5.Kuhifadhi kazi yake mara kwa mara.
6.Kuzima kompyuta kwa utaratibu baada ya matumizi.
ANGALIA VIDEO HII
MASWALI YA MAZOEZI
A. Jaza nafasi zilizo wazi
1.______ ni programu inayotumika kuchora kwenye kompyuta.
2.______ hutumika kufuta sehemu ya mchoro.
3.______ hutumika kuandika maneno kwenye picha.
4.______ hutumika kujaza eneo kwa rangi.
5.______ hutumika kuchora maumbo mbalimbali.
B. Jibu maswali
6.Paint ni nini?
7.Taja matumizi matatu ya Paint.
8.Taja vifaa vitano vinavyopatikana katika Paint.
9.Eraser hutumika kufanya nini?
10.Taja vitu vitatu vya Sayansi ambavyo mwanafunzi anaweza kuchora kwa kutumia Paint.
11.Taja faida mbili za kujifunza Paint.
12.Taja tahadhari mbili wakati wa kutumia kompyuta.
C. Kazi ya Vitendo
13.Tumia Paint kuchora mmea.
14.Weka rangi kwenye mchoro wako na 25.uandike majina ya sehemu zifuatazo:
Mizizi – Shina – Majani – Ua.
0 Comments: