Monday, July 20, 2026
*NECTA NECT NECTA NECTA NECTA NECTA NECTA*
*๐ข HII NI KUTOKA NECTA MABADILIKO MAPYA YA KAZIMRADI (PROJECTS) KATIKA SOMO LA BUSINESS STUDIES*
Habari za majukumu wanachama wa chaneli hii!
Leo tunaleta uchambuzi wa kina kuhusu mwongozo mpya wa Kazimradi (Project-Based Assessment - PBA) katika somo la *Business Studies* kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Lengo ni kuhakikisha kila mdau anafahamu wajibu wake, hatua za utekelezaji, pamoja na ratiba rasmi ili utekelezaji wa miradi hii uwe wenye mafanikio.
*๐ฏ LENGO KUU LA KAZIMRADI (PROJECTS)*
Kazimradi hizi zimeandaliwa na NECTA na kuwekwa kwenye tovuti yao pamoja na mfumo wa PReMS kwa wanafunzi wa:
✅ Kidato cha Kwanza
✅ Kidato cha Pili
✅ Kidato cha Tatu
Malengo ya Kazimradi:
๐ฅ Kumsaidia mwanafunzi kutumia maarifa ya biashara kutatua changamoto halisi za jamii.
๐ฅ Kukuza stadi za vitendo, ubunifu, ushirikiano, ujasiriamali, na fikra kinzani.
๐ฅ Kujenga uzalendo na uwajibikaji unaoendana na dira ya taifa ya maendeleo ya viwanda na kujiajiri.
*๐ MCHANGO WA ALAMA KWENYE MATOKEO YA MWISHO*
๐ Kazimradi hizi ni endelevu na zitafanyika kila muhula.
๐ Kazimradi ya Kidato cha Tatu Muhula wa Pili itakamilishwa mwanafunzi anapoingia Kidato cha Nne Muhula wa Kwanza.
๐ Katika somo la Business Studies, kazimradi itachangia jumla ya alama 7 katika Alama Endelevu (C.A) za mwanafunzi zitakazotumika kuchakata matokeo ya mwisho.
๐ Alama hizi ni mahsusi kwa somo la Business Studies pekee.
*๐ ️ MIONGOZO RASMI ILIYOTOLEWA NA NECTA*
NECTA imeandaa nyaraka mbili muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa PBA:
๐ Project Based Guidelines
๐ Project Based Implementation Manual
*Nyaraka hizi zinapatikana kupitia tovuti ya NECTA pamoja na mfumo wa PReMS.*
*๐ฅ WAJIBU WA WADAU MBALIMBALI*
⚡ 1. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)
๐น Kuratibu utekelezaji wa PBA kitaifa.
๐น Kusambaza miongozo rasmi ya miradi.
๐น Kuhakikisha miradi inaendana na mtaala na matokeo ya ujifunzaji.
๐น Kusimamia ukusanyaji, uhakiki, na utunzaji wa alama zote.
⚡ 2. Wakuu wa Shule*
๐น Kusimamia utekelezaji wa PBA ngazi ya shule.
๐น Kutoa msaada kwa walimu na kuhakikisha usahihi wa alama.
๐น Kuwasilisha matokeo yaliyohakikiwa kupitia mfumo wa PReMS.
⚡ 3. Walimu wa Taaluma*
๐น Kusimamia utekelezaji wa miradi kwa kuzingatia mtaala.
๐น Kutoa mwongozo kwa walimu wa somo.
๐น Kuhakikisha tathmini inafanyika kwa haki na usawa.
⚡ 4. Walimu wa Somo la Business Studies*
๐น Kutambulisha malengo, ratiba, na mahitaji ya miradi mwanzoni mwa muhula.
๐น Kusimamia na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kwa kutumia fomu maalumu.
๐น Kufanya tathmini kwa kutumia vigezo sanifu (rubrics) vya NECTA.
๐น Kukusanya na kuwasilisha alama kwa Mkuu wa Shule.
⚡ 5. Wanafunzi*
๐น Kushiriki kikamilifu katika kazi za vikundi.
๐น Kutumia maarifa ya biashara kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.
๐น Kuandaa na kuwasilisha miradi kwa njia ya:
- Ripoti za maandishi
- Mabango (posters)
- Mifumo ya kidijitali
*⏱️ MCHAKATO WA UTEKELEZAJI*
๐ Kazi za miradi zitafanyika kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8.
๐ Wanafunzi watakusanya taarifa, kufanya mahojiano, na kushirikiana katika vikundi.
๐ Miradi itawasilishwa mbele ya jopo la walimu na wadau husika kwa kutumia:
- Mabango
- Vielelezo (models)
- Ripoti
๐ Vigezo vya utoaji wa alama vitazingatia:
✅ Ubunifu
✅ Usahihi
✅ Mpangilio
✅ Mawasiliano
✅ Matumizi ya dhana za somo
*♿ USHIRIKISHWAJI WA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM*
Shule zinapaswa kuhakikisha usawa kwa:
✔ Kubadilisha majukumu ya miradi kulingana na aina ya ulemavu.
✔ Kutoa vifaa saidizi kama Braille au wakalimani.
✔ Kuruhusu muda wa ziada pale inapobidi.
✔ Kuwashirikisha walimu wa elimu maalum katika usimamizi.
*๐
KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MIRADI – MWAKA 2026*
๐ Kidato cha I, II & III (Muhula wa Kwanza)
๐️ Kutoa Kazimradi:
*09/03/2026 – 20/03/2026*
๐️ Utekelezaji:
*30/03/2026 – 05/04/2026*
๐️ Uwasilishaji:
*20/04/2026 – 30/04/2026*
๐️ Kupandisha Alama (PReMS):
*11/05/2026 – 29/05/2026*
๐ Kidato cha I & II (Muhula wa Pili)
๐️ Kutoa Kazimradi:
*17/08/2026 – 28/08/2026*
*๐️ Utekelezaji:*
07/09/2026 – 11/09/2026
(Kidato cha II hadi 09/09/2026)
*๐️ Uwasilishaji:*
28/09/2026 – 11/10/2026
๐️ Kupandisha Alama (PReMS):
14/10/2026 – 06/11/2026
*๐ Kidato cha III (Muhula wa Pili)*
๐️ Kutoa Kazimradi:
09/03/2026 – 20/03/2026
*๐️ Utekelezaji:*
07/09/2026 – 09/09/2026
*๐️ Uwasilishaji:*
28/09/2026 – 11/10/2026
*๐️ Kupandisha Alama (PReMS):*
14/10/2026 – 06/11/2026
*๐ HALI YA UPAKUAJI WA NYARAKA*
(Takwimu hadi 10/02/2026)
NECTA imebainisha kuwa kasi ya upakuaji wa nyaraka bado ni ndogo. Shule zinahimizwa kuchangamkia fursa hii mapema.
Mpaka mwezi Huu WA Tano 2026
๐ Shule zilizopakua miongozo (Guidelines & Manual):
2,230 tu (29.71%) kati ya shule 7,506.
๐ Shule zilizopakua Kazimradi (Projects):
1,332 tu (17.75%) kati ya shule 7,506.
๐ Shule zilizowasilisha alama za C.A kwenye mfumo wa PReMS:
355 tu (4.73%) kati ya shule 7,506.
*๐ก HITIMISHO*
Ufanisi wa utekelezaji wa Kazimradi hizi unategemea ushirikiano wa karibu kati ya:
๐ค Uongozi wa Shule
๐ค Walimu
๐ค Wanafunzi
Kila mdau anahimizwa kupitia miongozo hii kikamilifu kupitia tovuti ya NECTA ili kuhakikisha uadilifu, usawa, na mafanikio katika tathmini hii ya vitendo.
๐ข Sharing is Caring!
Tafadhali sambaza ujumbe huu kwa walimu na wadau wengine wa elimu ili sote twende sawa.
Imeandaliwa na
Mwalimu na Mifumo*
๐ 0753 538 043
Sunday, July 19, 2026
Top Computer Courses to Learn in 2026
If you want to improve your digital skills and boost your career, here are some of the best computer courses you can study:
1.Computer Applications – Learn Microsoft Word, Excel, PowerPoint, Access, Internet, and Email.
2.Computer Programming – Learn programming languages such as Python, Java, C++, and JavaScript.
3.Web Design and Development – Build modern websites using HTML, CSS, JavaScript, PHP, and databases.
4.Graphic Design – Create professional designs using Adobe Photoshop, Illustrator, and Canva.
5.Networking – Learn computer networking, network setup, and troubleshooting.
6.Cybersecurity – Understand how to protect computers, networks, and online information from cyber threats.
7.Database Management – Learn MySQL, SQL Server, Oracle, and database administration.
8.Data Analysis – Analyze and visualize data using Microsoft Excel, Power BI, Python, and SQL.
9.Digital Marketing – Learn SEO, social media marketing, Google Ads, email marketing, and content marketing.
10.Artificial Intelligence (AI) – Explore machine learning, AI tools, prompt engineering, and automation.
11.Mobile App Development – Develop Android and iOS applications using Flutter, Kotlin, or React Native.
12.Video Editing – Edit professional videos using Adobe Premiere Pro, CapCut, DaVinci Resolve, and After Effects.
13.Computer Hardware and Maintenance – Learn computer assembly, repair, maintenance, and troubleshooting.
14.Cloud Computing – Study cloud platforms such as AWS, Microsoft Azure, and Google Cloud.
15.UI/UX Design – Design user-friendly websites and mobile applications using Figma and Adobe XD.
These courses are suitable for students, teachers, job seekers, entrepreneurs, and professionals who want to improve their computer skills and increase their career opportunities in today's digital world.
Friday, July 17, 2026
Course ya computer application na faida zake
Computer Application ni kozi inayokufundisha jinsi ya kutumia kompyuta na programu mbalimbali zinazotumika ofisini, shuleni na kwenye biashara. Ni moja ya kozi rahisi kuanza nayo hata kama huna uzoefu mkubwa wa kompyuta.
Kwa kawaida utajifunza mambo kama:
1.Microsoft Word – kuandika na kupanga nyaraka.
2.Microsoft Excel – kutengeneza jedwali, kufanya mahesabu na kuchambua data.
3.Microsoft PowerPoint – kuandaa mawasilisho (presentations).
4.Microsoft Access – misingi ya hifadhidata (database).
5.Matumizi ya Internet, barua pepe (Email) na utafutaji wa taarifa mtandaoni.
6.Misingi ya matumizi ya mfumo wa uendeshaji kama Windows na usimamizi wa mafaili.
Faida za kozi hii
1.Inakupa ujuzi unaohitajika kwenye kazi nyingi za ofisini.
2.Huongeza nafasi za kupata ajira katika sekta mbalimbali.
3.Husaidia kuendesha biashara au kazi binafsi kwa ufanisi.
4.Ni msingi mzuri kabla ya kusoma kozi za juu kama IT, Programming au Networking.
Kwa Tanzania, kozi hii inaweza kuwa ya wiki chache, miezi 3–6, au zaidi, kutegemeana na chuo na kiwango cha mafunzo.



.jpg)