Sifa za viumbehai
Viumbehaihai hai wana sifa kuu saba ambazo ni
1.Kula: viumbehai wanahitaji chakula ili waendelee kuishi kwa kula vyakula vinavyotokana na mimea na wanyama.
2.Kupumua: Viumbehai vyote hupumua,wanyama huingiza gesi ya oksijeni na kutoa gesi ya kabonidayoksaidi wakati wa kupumua na mimea huingiza gesi ya kabonidayoksaidi wakati wa mchana na kutoa gesi ya oksijeni na wakati wa usiku mimea hutumia hewa ya oksijeni na kutoa hewa ya kabonidayoksaidi.
3.Kuitikia vichocheo:Viumbehai huitikia vichocheo kutoka ndani na nje ya mwili, Mfano wa vichocheo hivyo ni mwanga,joto,sauti,ladha na harufu. Wanyama huitikia vichocheo kwa kutumia milango ya fahamu kama vile pua, ngozi, macho, ulimi na masikio
4.kujongea: Viumbehai vyote hujogea. Kujongea kunahusisha kusogea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa wanyama hujogea kwa kutembea, kutambaa na kuruka ila kwa mimea hujogea kwa kubadili mwelekeo wa sehemu ya mmea kwa kupinda au kujizungusha kwenye kitu au mmea mwingine. Mmea hujogea taratibu sana kiasi kwamba ni vigumu kuona mjingeo huo kwa urahisi.
5.Kuzaliana:Uwepo wa Viumbehai vyote ni matokeo ya kuzaliana. Kuzaliana ni muhimu kwa mwendelezo wa vizazi
6.Kutoa takamwili:Viumbehai hutoa takamwili katika hali ya gesi na majimaji. Wanyama hutoa maji ya ziada na chumvichumvi nje ya mwili kwa njia ya mkojo na jasho, pia hutoa gesi kwa njia ya kupumua. Mimea hutoa takamwili katika hali ya maji, gesi, na utomvu kwa njia ya majani, shina au mizizi.
7:Kukua: Viumbehai wote hukua. Wanyama akiwemo binadamu hukua kwa kuongezeka kimo na uzito. Wanyama hupitia hatua mbalimbali za ukuaji mfano, utoto, ujana, utu uzima uzee na mimea hukua kwa kuongezeka kimo na uzito.
MAKUNDI MAKUU YA VIUMBEHAI
1.WANYAMA
Wanyama wamegawanyika katika makundi makuu mawili
(a) Wanyama wenye uti wa mgogo, ambao wamegawanyika katika makundi makuu matano ambayo ni samaki(viumbe wanaoishi ndani ya maji,kuna wanaoishi kwenye maji chumvi mfano papa na wanaoishi kwenye maji baridi sangara na kambale) amfibia(chura huishi majini katika hatua za awali za ukuaji),reptilia hujumuisha wanyama wote wanaoishi nchi kavu na majini (mamba, mjusi, Kobe, kenge, kasa na baadhi ya nyoka), ndege (hujumuisha wanyama wenye manyoya baadhi yao hufugwa na wengine huishi porini wengi wao huishi nchi kavu na baadhi huishi maji),Mamalia(viwele vya mamalia wa kike hutoa maziwa kwa ajili ya watoto wao.
2.MIMEA
Mimea imegawanyika katika makundi makuu manne ila hapa tutajifunza makundi mawili ambayo ni mimea inayotoa maua na mimea isiyotoa maua
(a) Mimea inayotoa maua
Ni ile ambayo ua ndio sehemu maalumu ya uzazi.
Ua hubadilika kuwa tunda na ndani ya tunda mbegu hukua na kukomaa mfano ngano,maharage,miembe,njegere na alizeti.Pia mimea hii imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Monokotiledoni(Monocotyledon) na Daikotiledoni(Dicotyledon)
1.Monokotiledoni
Ni Mimea ambayo ina ghala mbegu moja.mfanomtama,mahindi,ulezi,Nazi,ngano na majani yake yana vena zilizo sambaa kufuata urefu wa Jani, mizizi yake ni ya nyuzinyuzi na haina mzizi mkuu2.Daikotiledoni
Ni mimea ambayo ina ghala mbegu mbili.mfano miembe, maharage na kunde.Pia majani yake yana vena zilizotanda kama wavu na ina mzizi mkuu na mizizi mingine midogomidogoSEHEMU ZA MMEA
Mmea una sehemu kuu tatu ambazo ni mizizi,shina na majani.sehemu nyingine ni maua,matunda,na mbegu

Kazi za kila Sehemu ya mmea
Mizizi:-kufyonza maji na virutubisho kwenye udongo
-kushikiria mmea kwenye udongo ili usianguke
-kuhifadhi chakula kwa baadhi ya mimea mfano jaroti,mihogo na viazi vitamu

SHINA:-Kushikiria majani, maua na matunda
-kusafirisha maji, virutubisho na madini kutoka kwenye mizizi kwenda kwenye majani na matawi 

MAJANI:-Kutengeneza chakula cha mmea
-kudhibiti kiwango cha maji katika mmea kupitia stomata
-kuruhusu gesi ya oksijeni na kabonidayoksaidi kuingia na kutoka kwenye mmea
MATUNDA NA MAUA-Kazi kubwa ya maua ni uzazi, mmea huanzia kwenye mbegu.mbegu huota na kutoa mmea mchanga wenye majani.mmea ukisha komaa hutoa maua ambayo hutengeneza tunda.ndani ya tunda huwemo mbegu.ufuatao ni mchoro kuonyesha duru ya ukuaji wa mimea itoayo mbegu

Sehemu za nje za ua

Sehemu za nje na za ndani za ua

Mawasiliano yangu 0768569349/0628710705/0617430882
Email: enrickngwenya@gmail.com
Hotmail: enrickngwenya@hotmail.com
0 Comments: