Uchunguzi wa kisayansi
Ni kitendo cha kutafuta majibu ya maswali kwa kutumia mbinu mbalimbali za kitafiti.Utafiti unahusisha kutafuta taarifa kwa lengo la kujenga maarifa mapya au kuboresha maarifa yaliopo. Uchunguzi wa kisayansi hutumia njia na hatua zenye mpangilio maalumu ili kutafuta majibu ya maswali. Mfano wa maswali hayo ni kwa nini mtu huugua, kwa nini mvua hunyesha, kwa nini tunda hudondoka kwenye mti kuelekea chini.
Sababu za kufanya uchunguzi wa kisayansi
1.kutafuta majibu ya maswali ya kisayansi
2.kutafuta maarifa au mawazo mapya
3.kuthibitisha au kukanusha kanuni za kisayansi
4.kuthibitisha dhanio au kufafanua matukio ya asili
Mahitaji ya kufanyia uchunguzi wa kisayansi
1.viumbehai mfano mimea au sehemu za mmea na wanyama au sehemu za mnyama
2.vitu visivyo hai mfano udongo, mawe, maji, tindikari, nyongo
3.vifaa mbalimbali vya kupitia mfano futikamba, saa, mizani, kipimajoti, bika, lenzi, hadubini, chips, jokofu
4.vifaa vya kurekodia data wakati wa uchunguzi wa kisayansi mfano daftari kalamu, kalamu rashasha na penseli
HATUA ZA KUFANYA UCHUNGUZI WA KISAYANSI
1.Kubaini tatizo
2.kubuni dhanio
3.kuandaa mahitaji ya jaribio
4.kufanya jaribio na kukusanya data
5.kuchambua data
6.kutafsiri matokeo
7.hitimisho
8.Kuandaa taarifa
JINSI YA KUANDIKA TAARIFA YA UCHUNGUZI
1.Lengo/kusudi la uchunguzi
2.vifaa vilivyotumika katika uchunguzi
3.hatua/njia zilizotumika wakati wa kufanya uchunguzi
4.matokeo ya uchunguzi
5.hitimisho
0 Comments: