Ni mtiririko wa elektoni katika sakiti.nishati hii ni nishati inayoweza kubadilishwa kuwa aina nyingine ya nishati kama vile joto mwanga na sauti
AINA ZA UMEME
1.Umeme Tuli. 2.Umeme tiririka
UMEME TULI
Ni Umeme ambao hutokana na msuguano wa maada.mfano msuguano kati ya matone ya maji yaliopo angani kwenye mawingu na hewa husababisha mkusanyiko wa chaji katika mawingu. Mawingu hayo yanaposuguana husababisha kutokea kwa Radi. Hivyo radi ni umeme Tuli. Umeme tuli chaji zake hazitiririki.
UMEME TIRIRIKA
Ni Umeme ambao hutokana na mtiririko wa elektoni. Umeme tiririka ni waaina mbili ambao ni
1.umeme mkondo mnyoofu (DC)
2.umeme mkondo geu (AC)
Umeme tiririka huzalishwa kwa kutumia
(a) mitambo inayoendeshwa kwa nguvu za maji,upepo,fueli na gesi
(b) Nishati ya jua
(c)Seli kavu au seli za maji
(d) Dainamo ya baiskeli
SAKITI
Ni njia maalumu ya Umeme
AINA ZA SAKITI
1.Sakiti mfuatano 2.sakiti sambamba
1.SAKITI MFUATANO
Ni sakiti yenye njia moja tu ya Umeme
Hasara za sakiti hii
1.kikiza kimoja kikiungua kingine hakitaendelea kuwaka kwa sababu kuna mkondo mmoja tu wa umeme
2.kadri unavyoongeza vikinza voltage hupungua
2.SAKITI SAMBAMBA
Ni sakiti yenye njia zaidi ya moja ya Umeme
Faida za sakiti sambamba
1.kikinza kimoja kikiungua kingine kitaendelea kuwaka kwa sababu kuna mikondo tofauti ya umeme
2.kiasi cha voltage katika matawi yote ya sakiti kinalingana
3.ukinzani hupungua kadri unavyoongeza vikinza
Hasara za sakiti sambamba
1.sakiti inaweza kuzidiwa kwa sababu ya kuongezeka kwa mkondo wa umeme kwa kila kifaa kitumiacho umeme kinapoongezeka.
0 Comments: