
Katika Tanzania kuna baadhi ya maeneo yenye masalia ya kale kama vile
1.OLDUPAI(ARUSHA)
Neno oldupai ni neno lililotokana na kimasai likimaanisha katani kutokana na mwanaakiolojia kushindwa kutamka kama OLDUVAI GORGE, Hili ni eneo ambalo mwanaakiolojia Dkt Louis Leakey na mkewe Dkt Marry Leakey waligundua fuvu la binadamu wa kale lililoitwa Zinjanthropus liligunduliwa mwaka 1959
2.ENGALUKA(ARUSHA)
Hii ni sehemu ambayo masalia ya mifumo ya Kilimo cha umwagiliaji iliyotumika na watu wa kale ilihifadhiwa
3.AMBONI(TANGA)
Hii ni sehemu maarufu kwa kumbukumbu ya urithi wa historia ya Tanzania kwa kuwa na mapango mkubwa yenye maumbo mbalimbali ya kihistoria
4.ISIMILA(IRINGA)
Hili ni eneo lenye masalia ya zana za mawe za mwanzo zilizotumika na wakazi wa eneo hili
5.KILWA KISIWANI(LINDI)
Sehemu hii ni maarufu kwa kuwa na majengo ya kihistoria yaliyojengwa na waarabu ikiwemo misikiti
6.KAOLE NA MJI MKONGWE WA BAGAMOYO(PWANI)
Hili ni eneo la kihistoria ambapo hutunzwa kumbukumbu za kihistoria za mabaki ya masalia ya majengo ya misikiti na vito vya thamani kutokana Mashariki ya mbali na Asia.
7.KONDOA IRANGI(DODOMA)
Sehemu hii ni maarufu kwa kuwa na michoro mbalimbali ya mapangoni iliyochorwa katika miamba
0 Comments: