MASHINE
Ni kitu chochote kinachorahisiaha kazi.mashine imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni mashine rahisi na mashine tata.Mifano ya mashine rahisi ni koleo,nyundo,toroli,opena,mkasi,bembea, roda,mtange,mtaimbo na spana.mashine tata ni mashine zilizoundwa kutokana na mashine rahisi mbili au zaidi.Mfano wa mashine tata ni cherehani na baiskeli.
MASHINE RAHISI
Dhana ya mashine rahisi
Ni mashine za msingi ambazo ni wenzo,mteremko,kabari,gurudumu na ekseli,roda na skrubu.
Makundi ya mashine rahisi
Kuna makundi sita ya mashine rahisi ambayo ni wenzo, mteremko, kabari ,gurudumu na ekseli ,roda na skrubu
WENZO
Ni kundi la mashine rahisi ambayo hugeuka au kujizungusha kwenye sehemu iitwayo egemeo.wenzo inasehemu kuu tatu ambazo ni egemeo,jitihada na mzigo.mifano ya wenzo ni mtaimbo, koleo, nyundo ,toroli ,opena, mkasi, spana na sepeto.
MADARAJA YA WENZO
(a) wenzo daraja la kwanza
Katika nyenzo daraja la kwanza, egemeo huwa katikati ya mzigo na jitihada.mfano wa nyenzo daraja la kwanza ni mtaimbo, mtange, mkasi, nyundo na mizani
(b) Nyenzo daraja la pili
Katika nyenzo daraja la pili mzigo huwa katikati ya egemeo na jitihada.mfano wa nyenzo daraja la pili ni toroli na opena.
(c) Nyenzo daraja la tatu
Katika nyenzo daraja la tatu jitihada huwa katikati ya mzigo na egemeo.mifano ya nyenzo daraja la tatu ni kibanio cha mkaa.fagio la wima,doana ya kuvulia samaki na sepeto.
MATUMIZI YA NYENZO
1.kubeba mizigo
2.kung'orea misumari
3.kunyolea au kukatia vitu
4.
MTEREMKO
Ni ubao au CHUMA kilichowekwa kwa kuegemezwa upande mmoja ukiwa juu na mwingine ukiwa chini ya ule wa juu hivyo kutengeneza eneo lenye mteremko, aina hii ya mashine hutumika kupandishia au kushushia vitu kutoka sehemu iliyoinuka.Mfano wa mteremko ni ngazi,jembe la play, mchezo wa kuteleza na patasi.
KABARI
Ni kipande cha mti au chuma chenye kichwa kinene kwa upande mmoja na kuchongoka kuelekea sehemu ya makari.mfano wa kabari ni shoka ya chuma kabla haijawekwa mpini,makari ya patasi,kisu,sindano na kipande c
ha mti au chuma chenye ncha.
0 Comments: