🎓 TCU YAFUNGUA RASMI DIRISHA LA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA 2026/2027
💰 HESLB NAYO YAFUNGUA RASMI DIRISHA LA MAOMBI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU
*🎉 Habari njema kwa wahitimu wote!*
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza rasmi kufunguliwa kwa Dirisha la Maombi ya Udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
📅 Dirisha la Udahili
🟢 Limeanza: 10 Julai, 2026
🔴 Linafungwa: 10 Agosti, 2026
💰 Sambamba na hilo, HESLB nayo imefungua rasmi Dirisha la Maombi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
«⏳ Usisubiri siku za mwisho! Fanya maombi ya udahili na mkopo mapema ili kuepuka msongamano wa mfumo na makosa yanayoweza kujitokeza.»
👨🎓 Nani Anatakiwa Kuomba Udahili?
✅ Wahitimu wa Kidato cha Sita (ACSEE)
✅ Wahitimu wa Diploma (Stashahada)
✅ Wahitimu wa Foundation Certificate kutoka vyuo vinavyotambuliwa
📝 Hatua Muhimu za Kufanya Maombi ya Udahili
📌 Tembelea mfumo wa udahili wa chuo unachotaka kujiunga nacho.
📖 Soma kwa makini sifa za kozi unayotaka kuomba.
📝 Jaza taarifa zako kwa usahihi.
✔️ Hakikisha majina, matokeo na taarifa nyingine zinafanana na nyaraka rasmi.
📱 Tumia namba ya simu inayopatikana muda wote.
📧 Tumia barua pepe (Email) inayofanya kazi.
💰 Unataka Kuomba Mkopo wa HESLB?
🎯 Usisubiri mpaka upate udahili ndipo uanze kutafuta nyaraka. Ziandae mapema.
*📂 Nyaraka Muhimu za Kuwa Nazo*
📄 Cheti cha Kuzaliwa (Birth Certificate)
🆔 Namba ya NIDA (NIN)
🎓 Cheti cha Kidato cha Nne (CSEE)
🎓 Cheti cha Kidato cha Sita (ACSEE) au Diploma/Foundation kwa wanaostahili
📸 Passport Size yenye ubora mzuri
📱 Namba ya Simu inayotumika
📧 Barua Pepe (Email)
👨👩👧 Nyaraka za mzazi/mlezi endapo zitahitajika kulingana na mwongozo wa HESLB
💳 Fedha za kulipia ada ya maombi (Application Fee) kama ilivyoelekezwa na HESLB
⚠️ Mambo Muhimu ya Kuzingatia*
✅ Soma kwa makini miongozo ya TCU na HESLB kabla ya kuanza maombi.
✅ Hakikisha taarifa zote zinaendana na nyaraka zako rasmi.
✅ Epuka kutumia taarifa zisizo sahihi.
✅ Usisubiri siku za mwisho kwa kuwa mfumo unaweza kuwa na msongamano.
📚 PAKUA MIONGOZO RASMI YA TCU NA HESLB*
🎓 TCU Admission Guidebooks
📘 1. Bachelor's Degree Admission Guidebook (Kidato cha Sita)*
👇👇
📘 2. Bachelor's Degree Admission Guidebook (Diploma/Equivalent)*
👇👇
💰 HESLB Loan Application Guidelines*
📗 Bachelor Degree Loan Application Guideline*
*👇👇*
📗 Diploma Loan Application Guideline*
*👇👇*
*🌟 Samia Scholarship Application Guideline*
*👇👇*
*⚖️ Post Graduate Diploma in Legal Practice (Law School) Loan Guideline*
*👇👇*
https://www.heslb.go.tz/images/storage/downloads/1781870571_3-lawschool-guidelines-for-2026-2027.pdf
📅 Ratiba Muhimu
🟢 Kuanza Maombi ya Udahili: 10 Julai, 2026
🔴 Mwisho wa Maombi ya Udahili: 10 Agosti, 2026
💰 Dirisha la Maombi ya Mkopo HESLB: Lilishafunguliwa rasmi mapema Sana Mwezi June 2026
📢 Ujumbe kwa Wahitimu
🌟 Fanya maombi ya udahili na mkopo mapema.
🌟 Chagua kozi inayolingana na ufaulu na malengo yako.
🌟 Soma miongozo rasmi kabla ya kufanya maombi.
🌟 Andaa nyaraka zako zote mapema.
🌟 Shiriki taarifa hii kwa wahitimu wengine ili nao wapate fursa ya kujiunga na elimu ya juu na kuomba mkopo kwa wakati.
Imeandaliwa na Testme:
0 Comments: