JIOGRAFIA NA MAZINGIRA – DARASA LA TATU
SURA YA NNE
MADA: UHARIBIFU WA MAZINGIRA
A. Chagua jibu sahihi
1.Mazingira ni nini?
A. Vitu vinavyotuzunguka
B. Vitabu vya shule
C. Chakula pekee
D. Nguo tunazovaa
2. kati ya vifuatavyo husababisha uharibifu wa mazingira?
A. Kupanda miti
B. Kutupa taka ovyo
C. Kusafisha mazingira
D. Kutunza vyanzo vya maji
3.Kukata miti bila kupanda mingine husababisha nini?
A. Uharibifu wa mazingira
B. Usafi wa mazingira
C. Kuongezeka kwa misitu
D. Kuongezeka kwa mvua
4.Taka zinapaswa kutupwa wapi?
A. Barabarani
B. Mtoni
C. Kwenye sehemu maalumu za taka
D. Shambani
5.Kipi ni chanzo cha uchafuzi wa maji?
A. Kutupa taka mtoni
B. Kupanda miti
C. Kusafisha visima
D. Kuhifadhi maji
B. Jaza nafasi zilizo wazi
6.Tunapaswa __________ miti ili kulinda mazingira.
7.Kutupa taka ovyo husababisha __________ wa mazingira.
8.Maji machafu yanaweza kusababisha ______ kwa binadamu.
9.Tunapaswa kuweka mazingira yetu katika hali ya __________.
10.Kukata miti kwa wingi kunaweza kusababisha__wa udongo.
C. Jibu kwa kifupi
11.Taja sababu mbili za uharibifu wa mazingira.
12.Taja madhara mawili ya uharibifu wa mazingira.
13.Taja njia mbili za kutunza mazingira.
14.Kwa nini tunapaswa kupanda miti?
15.Tunawezaje kuzuia uchafuzi wa maji?
D. Oanisha maneno yaliyopo Orodha A na majibu sahihi katika Orodha B.
Orodha A Orodha B
16. Kukata miti A. Uchafuzi wa mazingira
17. Kupanda miti B. Kutunza mazingira
18. Kutupa taka mtoni C. Uharibifu wa misitu
19. Kusafisha mazingira D. Mazingira safi
E. Kweli au Si Kweli
20.Kupanda miti husaidia kutunza mazingira. __________
21.Kutupa taka ovyo ni njia nzuri ya kutunza mazingira. _______
22.Uharibifu wa mazingira unaweza kusababisha magonjwa __________
23.Tunapaswa kulinda mito na vyanzo vya maji. __________
24.Kukata miti yote ni jambo zuri kwa mazingira. __________
F. Maswali ya kufikiri
25.Ukiona mwanafunzi anatupa taka uwanjani, utamshauri afanye nini?
26.Taja mambo matatu unayoweza kufanya shuleni ili kutunza mazingira.
27.Ni nini kinaweza kutokea ikiwa watu wataendelea kukata miti bila kupanda miti mingine?
28.Eleza kwa nini mazingira safi ni muhimu kwa afya ya binadamu.
0 Comments: