Shule zote zifungwe November 13 / 2026
*📢 TAARIFA MUHIMU KWA WALIMU, WAKUU WA SHULE NA WATUMISHI WOTE WA ELIMU! 🎓📚*
🗓️ MABADILIKO YA TAREHE YA KUFUNGA SHULE ZA AWALI, MSINGI NA SEKONDARI TANZANIA BARA MWAKA 2026
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa waraka mpya kuhusu mabadiliko ya tarehe ya kufunga shule kwa mwaka 2026, kufuatia tahadhari ya uwezekano wa mvua kubwa zinazosababishwa na hali ya hewa ya El Niño.
*🌧️ KWA NINI MABADILIKO HAYA?*
Kutokana na utabiri wa hali ya hewa, kuna uwezekano wa mvua kubwa kati ya Oktoba na Desemba 2026. Hali hii inaweza kuathiri shughuli za shule, usalama wa wanafunzi, walimu na watumishi wengine.
*📌 RATIBA MPYA YA KUFUNGA SHULE*
❌ Tarehe ya awali: 04 Desemba 2026.
✅ Tarehe mpya: 13 Novemba 2026.
📚 Mabadiliko haya yanahusu shule zote za awali, msingi na sekondari Tanzania Bara kwa mwaka 2026.
*📅 MUHIMU KUZINGATIA*
- 🗓️ Waraka umeanza kutumika rasmi tarehe 01 Oktoba 2026.
*- 🏫 Shule zote zinapaswa kufungwa tarehe 13 Novemba 2026.*
- 📖 Mabadiliko haya yanalenga kulinda usalama na ustawi wa wanafunzi, walimu na watumishi wengine wa shule.
*⚠️ WITO KWA WAKUU WA SHULE NA MAAFISA ELIMU*
Ni muhimu kupanga upya ratiba za masomo na shughuli nyingine za shule ili kuzingatia tarehe mpya ya kufunga shule.
📲 MitihanitzApp
Taarifa, Teknolojia na Mafunzo kwa Walimu,Wanafunzi,Wazazi,Wadau wa Elimu na Watumishi wa Umma.
*Follow Channel Kwa Update zaidi.*
#ElimuTanzania #Walimu #TAMISEMI #WizaraYaElimu #KalendaYaMasomo #TaarifaMuhimu
Imeandaliwa na MitihanitzApp:
0 Comments: