Maeneo sita muhimu ambayo mtoa alama anapaswa kuzingatia ili kuwasilisha ujumbe kwa ufasaha ni kama ifuatavyo:
1 kuzingatia eneo la mijongeo mitatu;, yaani juu kichwani, chini kiunoni na upande wa mabega.
2. Kuzingatia mipaka ya eneo la uundaji;. Mtoa alama anatakiwa kuzingatia mipaka ya eneo lake, ambayo ni wima na ulalo yaani juu ya kichwa hadi kiunoni na kutoka bega moja hadi lingine
3. Kuzingatia usahihi wa mijongeo;. hapa mtoa alama anatakiwa kuzingatia mwendo wa mkono ambapo ni kasi, mwelekeo na umbo la mwendo wa mkono.
4. Kuzingatia maelezo ya alama;. Mtoa alama anapaswa kuzingatia jinsi anavyo elekeza mikono yake, mfano kiganja kutazama ndani, nje au chini.
5. Kuzingatia minyumbuliko ya uso;. Mfano kupepesa macho, kuinua nyusi, au kubadilika umbo la mdomo.
6 Kuzingatia mijongeo ya mwili.; mkao wa mabega, kichwa na mwili kwa ujumla ili kusaidia ufafanuzi wa alama.

0 Comments: