Friday, October 25, 2024

 Ripoti ya kawaida

Muundo wa ripoti ya kawaida

Ripoti ya kawaida sharti iwe na sehemu kuu nne; sehemu hizo ni:

1. Kichwa cha ripoti
  • Ripoti lazima iwe na kichwa cha habari; kichwa hicho huandikwa kwa maelezo machache, kwa herufi kubwa na kupigwa mstari.
  • Kichwa huoana na yanayoshughulikiwa. Kwa mfano: RIPOTI YA AJALI MBAYA YA GARIMOSHI
2. Utangulizi wa ripoti
  • Utangulizi wa ripoti hueleza kwa muhtasari lengo la ripoti kama ni kutoa taarifa au kumbukumbu.
3. Kiini cha ripoti/mwili
  • Kiini cha ripoti kina maelezo yote kuhusiana na tukio lenyewe; sehemu hii huelezea kwa ufasaha mambo yaliyotokea, chanzo chake, ukubwa wake, wahusika, na tukio linalohusika.
  • Ufafanuzi huu uwe ni wa ukweli wa kuaminika(si lazima iwe tukio la kweli lakini haistahili kumingisha mtu dhana ya uongo).
  • wakati uliopita nanafsi ya tatu hutumika isipokuwa unavyomnukuu myu moja kwa moja.
4. Mwisho wa ripoti
  • Hii ni sehemu ya mwisho ya ripoti. Sehemu hii huonyesha mambo makuu mawili:
  1. maoni/mapendekezo ya mwandishi wa ripoti.
  2. Lazima sentensi "Ripoti hii imeandaliwa na kuandikwa na:" iwe katika hitimisho, kisha kufuatwa na jina na cheo cha mwandishi pamoja

Msomihuru blog is an educational blog that provides clear, insightful, and practical knowledge on academics, society, technology, literature, science, and personal development. Learn freely, grow daily.

0 Comments: