Headlines
Loading...

Friday, October 25, 2024

JINSI YA KUANDIKA BARUA YA KIRAFIKI/KINDUGU

  • MADA YA 1: UANDISHI WA BARUA ZA KIRAFIKI, MWALIKO NA MATANGAZO

    Uwezo mahususi
    Kuandika barua za kirafiki, mwaliko na matangazo kwa watu mbalimbali

    Malengo ya ujifunzaji

    - Kutaja sehemu kuu za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo 
    - Kuchunguza muundo wa barua za kirafiki, mwaliko na matangazo
    - Kutofautisha aina za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo 
    - Kuelezea lugha inayofaa kutumiwa katika uandishi wa barua za kirafiki, 
    mwaliko na matangazo
    - Kutunga barua za kirafiki kwa watu mbalimbali, barua za mwaliko na 
    matangazo ya aina tofauti
    - Kuonyesha adabu na hehima kwa watu anaowaandikia

    - Kueleza matumizi ya aina za maneno

  • Hapa chini ni mfano wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko pamoja na maelezo ya kila sehemu.

    MUUNDO WA BARUA ZA KIRAFIKI

    Barua za kirafiki huundwa na mambo muhimu yafuatayo

    1. Anuani ya mwandishi
    2. Tarehe
    3. Mwanzo wa barua
    4. Kiini cha barua
    5. Mwisho wa barua
    6. Jina la Mwandishi


    1.ANUANI YA MWANDISHI

    –      Huandikwa juu kwenye pembe ya kulia ya karatasi. Huandikwa kwa waziwazi na kwa usahihi ili mwandikiwa aitumie kujibu barua aliyotumiwa

    –      Huweza kuandikwa kwa muundo wa mshazari au wima.


  • 2.TAREHE

    –      Huandikwa chini kwenye anuani ya mwandishi ili kumjulisha mwandikiwa lini barua imeandikwa

    –      Tarehe huweza kuandikwa kwa miundo mbalimbali mfano: – 2-02-2012, 02/02/2012, 2.2.2012 au february

    3.MWANZO WA BARUA

    Huandikwa kushoto chini ya mstari wa tarehe huweza kuandikwa kwa kutajwa jina, eneo au wadhifa wa mtu anayeandikiwa

  • 4.KIINI CHA BARUA

    Sehemu hii hueleza kusudi/lengo la mwandishi, huelezea kusudi lake la kuandika barua.

  • 5.MWISHO WA BARUA

Hapa huwa na salamu za maagano na salamu hizo kutegemea mwandishi na mwandikiwa, mwisho wa barua huwa na maneno yenye ladha na mvuto.

6.   JINA LA MWANDISHI

Ni muhimu mwandishi kuandika jina ili kumjulisha mwandikiwa barua imetoka kwa nani.

  • KIELELEZO CHA MUUNDO WA BARUA ZA KIRAFIKI


  • Mtaa wa Kijitonyama,
    S.L.P. 123,
    Dar es Salaam.
    04 Agosti 2026

    Mpendwa Rafiki Amina,

    Shikamoo. Natumaini unaendelea vizuri pamoja na familia yako. Mimi ni mzima wa afya na masomo yanaendelea vizuri.

    Ninakwandikia barua hii kukusalimia na kukujulisha kuwa likizo ijayo ningependa uje kunitembelea nyumbani kwetu. Tutapata nafasi ya kusoma pamoja, kubadilishana mawazo, na kufurahia likizo.

    Ninatumaini utapata nafasi ya kuja. Tafadhali wasalimie wazazi na ndugu zako wote kwa niaba yangu.

    Rafiki yako,

    Asha











0 Comments: