Thursday, December 19, 2024

TAWALA ZA KIKOLONI AFRIKA

Published from Blogger Prime Android App
MIFUMO YA TAWALA ZA KIKOLONI
Mifumo ya utawala wa kikoloni iliyotumiwa katika kuwatawala waafrika
(i) Mfumo wa utawala wa moja kwa moja(direct rule)
(ii) Mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma(indirect rule)
(iii) Mfumo wa utawala wa kulisha kasumba (Assimilation policy)
(iv) Mfumo wa kuheshimu utamaduni wa waafrika (A

I. MFUMO WA UTAWALA WA MOJA KWA MOJA (direct rule)
Ni Mfumo wa utawala ambao haukutumia viongozi wa jadi.

Sababu za kutumia Mfumo wa utawala wa moja kwa moja
-Wakoloni walifikiri Waafrika ni dhaifu katika uongozi
-Wakoloni walihisi waafrika si waaminifu
-Wakoloni waliwadharau waafrika na kuwaona si wastarabu
Mfumo huu wa utawala uliongozwa na Gavana aliyeitwa JULIUS VON SODEN

Sifa za Mfumo wa utawala wa moja kwa moja
-Mfumo ulitumiwa na Wajerumani
-Mfumo ulikuwa wa kikatili
-Mfumo ulitumia viongozi wachache wa kiafrika
-mfumo ulikuwa ghali kuuendesha
-mfumo haukuheshimu mila na desturi za Waafrika

ATHARI ZA MFUMO WA UTAWALA WA MOJA KWA MOJA
-mfumo Kuuwawa kikatili kwa waafrika
-Viongozi wa waafrika na wafuasi wa waafrika walibakwa,kukatwa viuongo na kuchapwa viboko hadharani
-mfumo Uliendeleza unyonyaji, ukandamizaji na unyanyasaji
-mfumo Ulivuruga Mfumo wa utawala wa kijadi

MFUMO WA UTAWALA WA MLANGO WA NYUMA
(Indirect rule)

Mfumo huu ulianzishwa mwaka 1914 na kapteni wa Uingereza aliyeitwa Frederick Lugard huko Nigeria kaskazini

Sababu za kutumia Mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma
-Uchache wa viongozi wa kizungu
-Kuogopa gharama za mfumo wa moja kwa moja
-Tatizo la lugha ya kuwasiliana
-Kupunguza lawama kwa serikali ya kikoloni
-Kurahisisha utekelezaji wa sera za kikoloni
-Kuwepo kwa magonjwa ya kitropiki mfano malaria

Sifa za Mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma
-Mfumo ulitumiwa na Waingereza
-mfumo haukuwa wa kikatili
-mfumo ulitumia viongozi wa jadi
-mfumo haukuwa na gharama
-mfumo uliheshimu mila na desturi za Waafrika

Athari za Mfumo wa utawala wa mlango wa nyuma
(a) Athari chanya(nzuri)
-Kuwepo kwa ufanisi katika utekelezaji wa maamuzi na malengo ya wakoloni
-Ulisaidia kupunguza gharama za utawala
-Uliheshimu tamaduni za AFRIKA
-Ulirahisisha mawasiliano kati ya wakoloni na waafrika

(b) Athari hasi(mbaya)
-Waafrika walipoteza uhuru wao
-Kuendeleza ukabaila
-Ulisababisha viongozi wa kiafrika walaumiwe

MFUMO WA UTAWALA WA KULISHA KASUMBA (ASSIMILATION POLICY)
Mfumo huu wa utawala ulitumiwa katika makoloni ya Wafaransa na wareno, Mfumo huu ulianzishwa huko Senegal baada ya Mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789

Sifa za Mfumo wa kulisha kasumba (Assimilation policy)
-Kubadilisha Mfumo wa maisha
-Kupunbaza Waafrika
-Waafrika wachache walisomeshwa
-Makoloni yalionekana kama majimbo ya Ufaransa
Matumizi ya lugha ya kifaransa

MFUMO WA UTAWALA WA KUHESHIMU UTAMADUNI WA MWAFRIKA
Katika mwaka 1910 Mfumo wa kulisha kasumba ulianza kukataliwa.

Sababu za kuanzisha Mfumo huu wa kuheshimu utamaduni wa waafrika
-Kuondoa upinzani wa waafrika
-Kupunguza gharama za utawala
-Baadhi ya Wafaransa hawakupenda kulinganishwa na waafrika

ATHARI ZA MFUMO WA UTAWALA WA KULISHA KASUMBA
-Ulidumaza mila na desturi za Waafrika
-Waafrika walifanywa wadharau na washindwe kuheshimu mila na desturi za Waafrika
-Waafrika walilazimishwa kufanya kazi
-Ulisababisha kuwepo kwa mazingira ya unyonyaji
-Kuzuka kwa migogoro kutokana na tofauti zao ususani Ukristo na Uislamu
-Waafrika waliopata elimu ya kifaransa walijiona ni Wafaransa


0 Comments:

Advertisement