Ni alama za msingi za mwongozo zinazotumika kuonesha uelekeo wa sehemu tofauti za dunia. Uelekeo huo ni kaskazini Kusini Mashariki na Magharibi. Alama za pande kuu za Dunia mara nyingi huoneshwa kwenye ramani dira na nyenzo mbalimbali za usafiri ili kumsaidia kufahamu eneo mahususi lilipo na kuweza kulifikia. Pande kuu za Dunia zinaunda msingi wa pande nyingine zaidi za dunia.
Mchoro kuonesha pande nne kuu za Dunia
NJIA ZA KUBAINI PANDE KUU NNE ZA DUNIA
Pande kuu za Dunia zinaweza kubainishwa kwa kutumia njia mbalimbali kama vile
(i) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia mawio na machweo ya jua
(ii) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia uelekeo wa kivuli
(iii) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia uelekeo wa nyota
(iv) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia ramani.
(v) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia dira
(i) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia mawio
Kuangalia jua linapochomoza wakati wa asubuhi na jioni unaweza kubaini pande kuu za Dunia. Hivyo wakati wa asubuhi ukisimama kuliangalia jua linapochomoza upande huo ni Mashariki na upande wako wa kulia huwa kusini na upande wako wa kushoto huwa kaskazini na Magharibi huwa nyuma ya mgongo wako. Vilevile ukisimama kuliangalia jua linapozama jioni upande huo ni Magharibi na upande wako wa kulia huwa kaskazini na upande wako wa kushoto huwa kusini.
(ii) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia uelekeo wa kivuli
Uelekeo wa kivuli chako wakati wa asubuhi na jioni unaweza kubaini pande kuu za dunia.Kwa kawaida unapotembea wakati wa asubuhi upande ambao kivuli chako kilipo ndio Magharibi na unapotembea wakati wa jioni upande ambao kivuli chako kilipo ndio Mashariki.
NB: Vigumu kufanya utambuzi wa pande kuu za Dunia wakati wa mchana kwa kuangalia uelekeo wa kivuli chako.
Picha ya kubaini pande kuu za dunia kwa Kutumia uelekeo wa kivuli
(iv) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia ramani
Ramani ni mwongozo mmojawapo unaotumika kubaini pande kuu za Dunia. Miongoni mwa vipengele muhimu vya ramani ni alama ya uelekeo wa kaskazini na hutumika kurahisisha kubaini pande kuu za Dunia yaani Kaskazini, Kusini ,Mashariki na Magharibi.
Mchoro wa ramani kuonesha uelekeo wa kaskazini
(v) Kubaini pande kuu za Dunia kwa Kutumia dira
Dira ni kifaa kinachotumiwa kutambua uelekeo wa kaskazini.Zipo aina mbili za dira ambazo ni
(i)Dira ya kidijitalia hutumia teknolojia kuonesha uelekeo na imeunganishwa kwenye GPS saa za kisasa simu janja na vyombo vya usafiri kama magari boti na ndege
(ii)Dira ya analojia ambayo hutumia vipande vya sumaku au sindano yenye sumaku kuelekeza upande wa kaskazini.
C
Mchoro kuonesha dira ya kidijitalia
PANDE NANE ZA DUNIA
Pande nane za Dunia hutoa mielekeo minne zaidi ya pande kuu za Dunia.Mielekeo hiyo ni Kaskazini -Mashariki, Kusini-Mashariki, Kusini -Magharibi na Kaskazini -Magharibi. Pande hizi zinatoa maelekezo ya kina au uelekeo mahususi na sahihi zaidi kuhusu mahali. Kwa kawaida hutumiwa katika nyanja mbalimbali kama vile usafiri wa anga au majini, jiografia na utabiri wa hali ya hewa
Mchoro kuonesha pande nane za Dunia
UMUHIMU WA PANDE NANE ZA DUNIA
1.Husaidia kubaini uelekeo wa mahali katika ramani na uso wa dunia
2.Huwasaidia wahandisi na wasanifu majengo katika kufanya ubunifu wa majengo, Barabara na reli.
3.Husaidia katika kuongoza vyombo vya usafiri
4.Husaidia kuimarisha ulinzi na usalama.
0 Comments: