Friday, February 14, 2025

UTAMADUNI WA MTANZANIA

UTAMADUNI
Maana ya Utamaduni
Ni mfumo mzima wa maisha ya watu fulani,jamii au nchi,mila na desturi zao za asili,jadi au Imani.Utamaduni hutambulisha na kuwaunganisha watu wa jamii husika kwa njia ya lugha, chakula,mavazi, nyimbo, michezo, Mila na desturi.

UTAMADUNI WA MTANZANIA
Ni mfumo wa maisha ya watanzani jinsi wanavyoishi kwa kufuata mila, desturi,jadi, Imani michezo na maendeleo yao kijamii,kiuchumi na kisiasa.Tanzania inamakabila yasiyopungua 120 yote yana mila na desturi zao za namna tofauti.Aidha utamaduni wa MTANZANIA umeunganishwa na lugha moja ya kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa na ni lugha ya mawasiliano katika nchi za Afrika ya Mashariki.

VIELELEZO VYA UTAMADUNI WA MTANZANIA
Utamaduni wa Mtanzania unajitokeza katika mambo mbalimbali kama vile lugha,mila, desturi, michezo, Sanaa na mavazi.

LUGHA:Ni chombo cha mawasiliano ambacho hutumika kama utambulisho wa jamii katika kuelimisha,kupashana habari na kubadilishana mawazi

MILA:Ni jumla ya mambo yanayofanywa na jamii husika kulingana na asili, mazingira na mienendo ya jamii hiyo.mfano wa mila ni jando na unyago

DESTURI:Ni mambo ya kawaida yanayofanywa mara kwa mara na wanajamii;Pia huweza kubadilika kulingana na mahali na wakati.mfano jamii zingine hutambuliwa kulingana na mavazi,vinywaji na vyakula

MICHEZO:Ni mambo yafanywayo kwa ajili ya kujifurahisha,kujichangamsha au kupitisha wakati.kwa Tanzania kuna aina mbili za michezo ambayo ni michezo ya jadi na michezo ya kisasa.michezo ya jadi ni kama vile kurusha mkuki,kucheza BAO,kukimbia,kubembea na kuruka Jamba.michezo ya kisasa ni kama vile mchezo wa ngumi, mchezo wa kuogelea na michezo mingine.

SANAA:Ni ufundi anaoutumia mtu ili kuwakilisha fikra au mawazo yake katika namna inayoburudisha na kufikirisha.tunaweza kuiona kazi ya sanaa kupitia fasihi,uchoraji,ususi,ushonaji,uchongaji na ufinyanzi
Sanaa hizi zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni

(a) Sanaa za maonyesho mara nyingi huoneshwa kwa umbo maalumu za zinaweza kuhifadhiwa kwa matumizi ya baadaye.mfano ufinyanzi.

(b)Sanaa ghibu ni zile sanaa zisizoonekana katika umbo maalumu au kushikika bali hugusa hisia mfano ushairi,uimbaji na muziki.

(c)Sanaa za vitendo huonekana katika uzuri wa umbo na hufanyika kwa vitendo mfano uigizaji,vichekesho,majigambo na nyimbo

UMUHIMU WA UTAMADUNI KWA MTANZANIA
1.Ni alama ya umoja wa kitaifa na utambulisho wa jamii.
2.Hudumisha uhusiano katika jamii kwa kutunziana heshima iliyopo
3.Husaidia jamii kuthamini rasilimali za Taifa letu
4.Hutunza maadili ya malezi ya watoto,vijana na wazee
5.Husisitiza uvaaji wa mavazi ya heshima
6.Hususitiza uwajibikaji miongoni mwa wanajamii ili kukuza uchumi
7.Huepusha kudharau tamaduni zetu na kuiga za kigeni
UMUHIMU WA MILA NA DESTURI
1.Kusisitiza kushiriki katika kufanya kazi kwa juhudi na maarifa
2.Kusaidiana na kutatua migogoro ya jamii
3.Kukemea kuiga tamaduni za kigeni zinazokwenda kinyume na tamaduni zetu
4.Kusaidia kuendeleza mila na desturi nzuri kwa Taifa
5.Kujenga ari ya kujitegemea

MAMBO YANAYOATHIRI UTAMADUNI
1.Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaweza kuathiri utamaduni
2.Mabadiliko ya mazingira kama vile ukame huathiri uzalishaji wa mazao hasa chakula
3.Kukua kwa lugha ya kiswahili kumechangia katika kuathiri lugha za makabila mengi
4.Mwingiliano baina ya nchi yetu na mataifa ya kigeni
5.Kushamiri kwa vipindi vingi visivyokuwa na maadili ya kitanzani katika televisheni,redio,magazeti na mitandao ya kijamii

NAMNA YA KUDUMISHA MILA NA DESTURI NZURI
1.Wazee wanapaswa kutumiwa kikamilifu kukusanya taarifa za jamii husika
2.Wazee wanapaswa kuweka mikakati ya kutangaza mila na desturi zao za zamani ili watanzani wengine wazitambue
3.Kuweka mikakati ya kuanzisha vituo vya kuhifadhi taarifa mbalimbali kuhusu mila na desturi za kila kabila

0 Comments:

Advertisement