Wednesday, April 2, 2025

HEWA NA UMUHIMU WAKE

HEWA
Ni mchanganyiko wa gesi mbalimbali zinazozunguka katika anga hewa.
Gesi zinazounda hewa
i.Naitrojeni 78%
ii.Oksijeni 20.9%
iii.Kaboni dayoksaidi 0.03%
iv.Agoni 0.90%
v.Gesi ningine 0.17%
SIFA ZA HEWA
1.Hewa ni maada isiyoonekana
2.Hewa inachukuwa nafasi ikiwekwa kwenye vifaa(mitungi ya gesi)
3.Hewa ipo katika hali ya gesi
4.Hewa haina harufu
5.Hewa haina rangi
6.Hewa inauzito inapojazwa katika kifaa maalumu
UMUHIMU WA HEWA
1.Husaidia uhai wa viumbe hai
2.Hutumika kuunguza vitu
3.Hutumika katika uchavushaji
4.Hewa hutumika kuzalishia umeme
5.Hewa hutumika kukaushia vitu
6.Hewa hutumika kusafirisha mawimbi ya sauti
7.Hewa husaidia kupaa na kuelea kwa vitu
8.Hewa hutumika kujaza kwenye matairi ya vyombo vya usafiri
9.Hewa husaidia kusawazisha kiwango cha jotoridi la Dunia
10.Hewa ni chanzo cha mvua

OKSIJENI
Ni gesi ambayo huchangia 20.9% katika hewa kutoka katika mimea,kwa kifupi huandikwa
        H2O+CO2   mwanga wa jua     O2+Kabohaidreti  
                                    Umbijani
Kanuni kanuni hii huitwa Usanisinuru au fotothinsesisi(photosynthesis)
UMUHIMU WA OKSIJENI
1.Husaidia katika upimaji
2.Hutumiwa na wasafiri wa anga
3.Hutumiwa viwandani katika uchomeleaji
4.Hutumiwa hospitalini kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa kupumua
5.Hutumiwa katika vyombo vya usafiri katika kuunguza mafuta
6.Hutumika katika usafirishaji wa maji taka
7.Hutumika kuwashia moto

KABONIDAYOKSAIDI
Ni hewa ambayo huzalishwa na viumbe hai,pia huzalishwa kwa kiasi kikubwa kutoka viwandani.kaboni dayoksaidi pia huitwa hewa ya UKAA.
UMUHIMU WA HEWA YA KABONIDAYOKSAIDI
1.Hutumika katika usanisi wa chakula cha mmea
2.Hutumika kugandisha vitu katika majokofu
3.Hutumika kuzimia moto
4.Hutumika kutengenezea mbolea za chumvi chumvi
5.Hutumika kuumulua mikate
6.Hutumika kutengenezea vivywaji mfano soda

ATHARI ZA HEWA YA KABONIDAYOKSAIDI
1.Husababisha Ongezeko la hali joto Dunia
2.Husababisha Kuongezeka kwa kina cha bahari
3.Husababisha mabadiliko ya tabia ya nchi
4.Husababisha maginjwa (Kansas)
GESI YA NITROJENI
Ni gesi ambayo huchangia 78% katika hewa.gesi hii huzalishwa kwenye shughuli za ikolojia,kilimo,ufugaji na uchafu mijini.
UMUHIMU WA GESI YA NITROJENI
1.Hutumika katika utengenezaji wa protini katika mimea na wanyama
2.Hutumika kutengenezea mbolea za chumvi chumvi mfano DAP,NPK,CAN,Yurea
3.Hutumika kutengenezea asidi iitwayo nitriki,rangi mbalimbali na nailoni
4.Hutumika hospitali kuhifadhia vitu mbalimbali kama mbegu na mayai ya uzazi,seli,neva na damu
5.Hutumika kuhifadhi vitu katika halijoto maalumu.
AGONI
Hii ni gesi bwete inayopatikana hewani.Agoni pamoja na gesi bwete nyingine huunda 0.90% ya hewa.Gesi hii huitwa gesi bwete kwa sababu haichanganyiki na elementi nyingine kutengeneza kampaundi

MATUMIZI YA GESI YA AGONI
1.Hutumika kwenye taa za umeme na neli ng'aavu za taa za umeme
2.Hutumika katika Kukata na kuchomelea vyuma katika vyombo vya usafiri kama magari

0 Comments:

Advertisement