Saturday, June 14, 2025

Mwanamke Mjamzito Na Kazi Zenye Madhara Kwa Mtoto Alie Tumboni.


pregnant-woma

Ni ukweli usio pingika kabisa kuwa, wanawake ni viumbe waliojaaliwa ujasiri wa kufanya kazi yoyote ambayo inaweza kufanywa na mwanaume, hii ni kutokana na kujijengea ujasiri huo kulingana na mazingira husika na ugumu wa maisha unaowakabili.

Ila uwezo wa kufanya kazi hizo inabidi uangalie pia na hali ya mwanamke huyo. Yeye anaweza kuona anafaa kwa kazi yoyote lakini mtoto alie tumboni angesema kuwa kazi afanyazo mama zinamdhuru au la endapo angekuwa na uwezo wa kufanya hivo.
Published from Blogger Prime Android App

Kwa kawaida ujauzito wa mwanadamu huweza kudumu kwa muda wa wiki 40, katika wiki hizo ndipo mabadiliko ya mtoto yanapotokea, kabla ya mama kujifungua. kuna hatua kuu tatu ambazo ujauzito hupitia. na katika kila hatua hizo kuna aina ya kazi au vitu vya muhimu na  ambavyo si vya muhimu kwa mwanamke mjamzito kuvifanya.

Hatua Za Ujauzito

Hatua Ya Kwanza- hii inaanzia wiki ya kwanza (1) hadi wiki ya  kumi na mbili (12). Hii ni hatua ya utambulisho kwa mwanamke kuwa ana ujauzito. Ni vizuri kwa mwanamke kufanya mazoezi na kula vyakul vizuri. Hapa unaweza hisi uchovu na kupata haja ndogo mara kwa mara. Kupungua au kuongezeka unene. Pia unaweza fanya kazi za kawaida kulingana na vile unajisikia.

Hatua ya pili- hii inaanza wiki ya kumi na tatu (13) hadi wiki ya 28. Kichefu chefu na kutapika kunaweza potea, kupinda kidogo kwa mgongo, pamoja na maumivu kiasi. kusinyaa kwa baadhi ya sehemu za mwili. hapa sasa haitakiwi kufanya kazi ngumu na za kukufanya usimame kwa muda mrefu.

Hatua ya tatu- hii huanzia wiki ya ishirini na tisa (29) hadi wiki ya mwisho ya kujifungua wiki ya 40. Hapa unahitaji muda mwingi wa kupumzika. Chuo kikuu cha YALE kimetoa tafiti kuwa asilimia 60 ya wanawake wajawazito wanasumbuliwa na maumivu ya mgogongo wanapotaka kulala. Lala kwa mkono wako wa kushoto kupunguza tatizo hili.
Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu hatua za mimba bofya hapa

Hivo basi aina ya kazi zinaweza kuleta madhara tofauti tofauti kwa kiumbe alie tumboni. Kwa namna hiyo basi, nimegawanya kazi hizo katika makundi matano kama ifuatavyo;-

Kazi Zenye Madhara Kwa Mtoto Alie Tumboni.
1.Kazi zinazohusu kusimama kwa muda mrefu.  Hizi ni zile kazi ambazo zinamfanya mama asipate muda wa kutosha wa kupumzika, kama vile mama anaefanya kazi ya kuuza mgahawa, ni wazi kabisa kuwa kazi hii inamuhitaji kusimama kuanzia jua linapochomoza hadi pale linapozama.

2.Kazi zinazohusisha madawa makali sana kama vile sumu. Hii inahusu kazi zile ambazo zinahusu utengenezaji wa kemikali au madawa yenye sumu, mfano mama mjamzito anaefanya kazi katika kiwanda cha utengenezaji sigara, ambapo anakumbana na harufu kali ya tumbaku na moshi pia.

3.Kazi zenye kuhitaji nguvu nyingi. Hizi ni zile kazi ambazo kuzifanya inabidi uwe umeshiba na una nguvu za kutosha. Mfano wa kazi hizo ni kusukuma toroli, kulima, kunyenyua mizigo mizito n.k.
Kazi zenye kuhusisha kutembea umbali mrefu. Hizi ni zile kazi ambazo mama mjamzito anazifanya ila kwa kutembea umbali mrefu. Mfano Kutembeza bidhaa kama vyombo, mboga mboga n.k.

4.Kazi za kuongea sana na kutumia viungo vya mwili pamoja na kusimama juani kwa muda mrefu. Mama mjamzito anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika na kufurahi na si kuongea sana wala kusimama juani.

Ni furaha kwangu kuona umepata elimu, tafadhali share ujumbe huu na marafiki au kama una swali lolote au maoni usisite kuandika hapo chini, asante sana.

Tags: Elimu na Afya
 
Ip man
Hey there, its ElimikaLeo blog here, thank you for visiting my blog.



0 Comments:

Advertisement