Msomi Huru

Headlines
Loading...
Advertisement

Oct 25, 2024

JINSI YA KUANDIKA BARUA RASMI/KIKAZI

Barua rasmi ni aina ya mawasiliano inayotumika katika muktadha wa kitaaluma au kiofisi. Ni muhimu kuandika barua hizi kwa umakini na kufuata taratibu maalum ili kuakisi heshima na taaluma. Hapa chini ni muundo wa barua rasmi pamoja na maelezo ya vipengele vyake muhimu.

Vipengele Muhimu vya Barua Rasmi

  1. Anwani ya Mwandishi
    • Anwani ya mwandishi huandikwa juu upande wa kulia wa karatasi. Hii inajumuisha jina la mwandishi, anuani ya posta, na nambari ya simu au barua pepe ikiwa ni lazima.
  2. Tarehe
    • Tarehe ya kuandika barua huandikwa chini ya anwani ya mwandishi, upande wa kulia wa karatasi.
  3. Anwani ya Mwandikiwa
    • Jina na cheo cha mwandikiwa, pamoja na anuani ya posta, huandikwa upande wa kushoto wa karatasi, chini ya tarehe.
  4. Salamu
    • Salamu rasmi kama “Ndugu” au “Mheshimiwa” ikifuatiwa na jina la mwandikiwa.
  5. Mada ya Barua
    • Mada ya barua inaweza kuandikwa kwa herufi kubwa na inapaswa kuwa fupi na kueleweka.
  6. Mwili wa Barua
    • Huu ni sehemu kuu ya barua ambapo mwandishi anaelezea madhumuni ya barua. Inajumuisha utangulizi, maelezo ya kina, na hitimisho.
  7. Hitimisho
    • Maneno ya shukrani au matarajio ya majibu yanaweza kujumuishwa hapa.
  8. Sahihi
    • Jina la mwandishi pamoja na sahihi yake huandikwa hapa. Cheo cha mwandishi kinaweza kujumuishwa ikiwa ni muhimu.
    • Published from Blogger Prime Android App

Mfano wa Muundo wa Barua Rasmi

Sehemu ya BaruaMaelezo
Anwani ya MwandishiJina la Mwandishi, S.L.P. 40, TUNNDURU 
Tarehe22 oktoba 2024
Anwani ya MwandikiwaJina la Mwandikiwa, S.L.P. 275, TUNNDURU 
SalamuMheshimiwa John Doe,
MadaMAOMBI YA KAZI
Mwili wa BaruaNinakuandikia barua hii kuomba nafasi ya kazi iliyotangazwa. Nina uzoefu wa miaka mitano katika…
HitimishoAsante kwa kuzingatia barua yangu. Natumaini kusikia kutoka kwako hivi karibuni.
SahihiMaria Mwema

Kuandika Barua Rasmi

  • Lugha Rasmi: Tumia lugha ya heshima na epuka maneno ya mazungumzo.
  • Uwazi: Andika kwa ufupi na kwa uwazi ili ujumbe uweze kueleweka kwa urahisi.
  • Usahihi: Hakikisha barua haina makosa ya tahajia au sarufi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuandika barua rasmi, unaweza kusoma hapa kwa mwongozo wa viwango na ushauri wa barua rasmi.

Pia, tembelea hapa kwa maelezo ya kina kuhusu utungaji wa barua rasmi. Ili kuelewa zaidi kuhusu aina na matumizi ya barua rasmi, angalia hapa.

JINSI YA KUANDIKA BARUA YA KIRAFIKI/KINDUGU
  • MADA YA 1: UANDISHI WA BARUA ZA KIRAFIKI, MWALIKO NA MATANGAZO

    Uwezo mahususi
    Kuandika barua za kirafiki, mwaliko na matangazo kwa watu mbalimbali

    Malengo ya ujifunzaji

    - Kutaja sehemu kuu za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo 
    - Kuchunguza muundo wa barua za kirafiki, mwaliko na matangazo
    - Kutofautisha aina za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo 
    - Kuelezea lugha inayofaa kutumiwa katika uandishi wa barua za kirafiki, 
    mwaliko na matangazo
    - Kutunga barua za kirafiki kwa watu mbalimbali, barua za mwaliko na 
    matangazo ya aina tofauti
    - Kuonyesha adabu na hehima kwa watu anaowaandikia

    - Kueleza matumizi ya aina za maneno

  • Hapa chini ni mfano wa barua ya kirafiki ya kutoa mwaliko pamoja na maelezo ya kila sehemu.

    Muundo wa Barua ya Kirafiki ya Kutoa Mwaliko

    1. Anwani ya Mwandikaji na Tarehe
    2. Mtajo
    3. Utangulizi
    4. Mwili wa Barua
    5. Tamati/Hitimisho
    6. Wasaalam

    Mfano wa Barua

    Anwani ya Mwandikaji na Tarehe

    Published from Blogger Prime Android App

    Maelezo ya Sehemu za Barua

    SehemuMaelezo
    Anwani ya Mwandikaji na TareheAnwani ya mwandishi huandikwa juu upande wa kulia wa karatasi. Tarehe huandikwa chini ya anwani.
    MtajoHuandikwa upande wa kushoto, chini ya tarehe. Huu ni utambulisho wa anayeandikiwa barua.
    UtanguliziHuu ni mwanzo wa barua unaojumuisha salamu na kujuliana hali.
    Mwili wa BaruaHuu ni sehemu kuu ya barua inayojumuisha sababu ya kuandika barua (mwaliko).
    Tamati/HitimishoHutoa salamu za mwisho, ushauri, maagano na kutakiana la heri.
    WasaalamHapa mwandishi huandika jina lake na uhusiano wake na mwandikiwa.
JINSI YA KUANDIKA RIPOTI

 Ripoti ya kawaida

Muundo wa ripoti ya kawaida

Ripoti ya kawaida sharti iwe na sehemu kuu nne; sehemu hizo ni:

1. Kichwa cha ripoti
  • Ripoti lazima iwe na kichwa cha habari; kichwa hicho huandikwa kwa maelezo machache, kwa herufi kubwa na kupigwa mstari.
  • Kichwa huoana na yanayoshughulikiwa. Kwa mfano: RIPOTI YA AJALI MBAYA YA GARIMOSHI
2. Utangulizi wa ripoti
  • Utangulizi wa ripoti hueleza kwa muhtasari lengo la ripoti kama ni kutoa taarifa au kumbukumbu.
3. Kiini cha ripoti/mwili
  • Kiini cha ripoti kina maelezo yote kuhusiana na tukio lenyewe; sehemu hii huelezea kwa ufasaha mambo yaliyotokea, chanzo chake, ukubwa wake, wahusika, na tukio linalohusika.
  • Ufafanuzi huu uwe ni wa ukweli wa kuaminika(si lazima iwe tukio la kweli lakini haistahili kumingisha mtu dhana ya uongo).
  • wakati uliopita nanafsi ya tatu hutumika isipokuwa unavyomnukuu myu moja kwa moja.
4. Mwisho wa ripoti
  • Hii ni sehemu ya mwisho ya ripoti. Sehemu hii huonyesha mambo makuu mawili:
  1. maoni/mapendekezo ya mwandishi wa ripoti.
  2. Lazima sentensi "Ripoti hii imeandaliwa na kuandikwa na:" iwe katika hitimisho, kisha kufuatwa na jina na cheo cha mwandishi pamoja
JINSI YA KUANDIKA CV NZURI YA KIINGEREZA


CURRICULUM VITAE OF MEINRAD MEINRAD NGWENYA
Particulars
Name: Meinrad meinrad ngwenya
Marital status: Married
E-mail: enrickngwenya@gmail.com,
Telephone: 0628710705
Nationality: Tanzanian
Date of birth: 18/07/1989

PROFILE
I am a creative, influential, corporative and enthusiastic person with well-organized performance, intellectual and competence in the areas of health.
Academic Background
Duration
Institute attended
Award
2010-2012
Mbeya Lutherani Teachers college 
Certificate of Primary Education
2009-2010Beroya Secondary SchoolAdvanced Certificate of Secondary Education (ACSE)
2005-2008St.Benedict Secondary SchoolCertificate of Secondary Education(CSE)
1998-2004
Mapinduzi Primary SchoolCertificate of Primary Education

Work experience
Place: Mlimareli Primary school in Mbalizi Mbeya
Position: Teacher
Date: February 2010– February 2010
Place: Bondeni Primary school in Mbozi
Position: Teacher
Date: February 2012- February 2012
Language Proficiency
Swahili: Excellent written and oral skills.
English: Excellent written and oral skills.
Skills
- Presentation and teaching skills.
- Communication skills.
- Good interpersonal skills.
- Computer literate: competent in MS Word, MS Excel, MS Publisher, MS PowerPoint.

Interests
Teaching, social networks, creative writing, music, reading books, football, swimming, playing game.
Referee available on request
Teacher Kavindi,
Head of school in Nampungu ,
Email: nampunguprimary2@gmail.com,
P.O.BOX 40,
Contact: 0768569349,
TUNDURU-RUVUMA.

Sophia Said Kapolo,
P. O. Box 275,
TUNDURU-RUVUMA.
Declaration
I, MEINRAD MEINRAD NGWENYA , do hereby declare and state that, the information given on this curriculum vitae is true to the best of my knowledge.