Thursday, November 21, 2024

SARATANI(CANCER)

SARATANI ni mkusanyiko wa seli zinazoongezeka bila kufuata utaratibu wa kawaida wa mwili. Seli za saratani huota haraka na kusababisha uvimbe

Kuna aina nyingi za saratani mfano
1.saratani ya shingo ya kizazi ambayo huwapata wanawake tu
2.saratani ya matini
3.saratani ya mapafu ambayo huwapata hasa wavutaji wa sigara
4.saratani za tumbo, utumbo mkubwa na ndogo, ngozi, damu, macho na Koo

Uvimbe wa saratani unaweza kupasuka na seli zake zikaingia kwenye damu. Kisha seli hizo zinaweza kusafirishwa na kwenda kujishikiza sehemu nyingine za mwili na hapo huweza kuanzisha uvimbe sehemu nyingine.

Chanzo halisi cha saratani hakijajulikana hadi sasa. Hata hivyo vipo vitendo mbalimbali vinavyoweza kuchangia kutokea kwa saratani mwilini. Vitendo hivyo ni uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi na kutokula matunda na vyakula vyenye nyuzinyuzi, kama vile nafaka zisizokobolewa na mbogamboga, kula vyakula vilivyokobolewa na kuongezwa kemikali, kukaa juani na kupigwa na mionzi mikali ya jua na uasherati

Dalili za saratani
-homa, uchovu kupitia kiasi, kupungua uzito, uvimbe na maumivu,
NB:dalili hizi zinaweza kuwa za magonjwa mengine mbalimbali,vipimo vya hospitali tu ndivyo vitakavyothibitisha endapo mtu ana saratani au la

Kinga na tiba ya saratani
  • Ugonjwa wa saratani unaweza kuzuilika kwa kuepuka vitendo vinavyochangia kupata saratani,kwa mfano uvutaji wa sigara na ulevi
  • Ugonjwa huu ukiwahi unaweza kutibika hospitalini kwa njia ya operation,mionzi au kemikali na
  • Ulaji wa chakula bora ni njia nzuri ya kuepuka saratani

0 Comments:

Advertisement