MTANDAO WA TARAKIRISHI
Ni mfumo ambao tarakirishi huunganishwa ili kuchangia vitumi,mafaili,printa au taarifa mbalimbali.Mtandao huu huundwa na tarakirishi mbili au zaidi kwa Kutumia waya au bila waya.
Vitumi vinavyounda mtandao
Mtandao huundwa na teknolojia mbalimbali zinazojumuisha maunzi programu na nyaya. Teknolojia hizo huunganisha tarakilishi na kuziwezesha kuwasiliana kubadilishana taarifa au data na kushirikiana katika kutumia rasilimali kama vile printa. Baadhi ya vitumi vinavyotumika kuunda mtandao ni tarakilishi, ruta, madaraja, swichi na nyaya.

Kielelezo cha vitumi vya mtandao
Faida za mtandao wa tarakilishi
Matumizi ya mtandao yana faida nyingi. Baadhi ya faida hizo ni:
1. Kushirikishana data na taarifa kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka tarakilishi moja kwenda nyingine.
2. Kutumia rasilimali na miundombinu kwa ushirikiano na kupunguza gharama za uendeshaji. Mfano, matumizi ya printa moja iliyounganishwa kwenye mtandao wa tarakilishi mbili au zaidi.
3. Kushirikiana katika kutumia programu, hivyo kupunguza gharama ya kununua maunzi kwa kila tarakilishi. Mfano, gharama ya kununua programu ya kuzula virusi vya mtandao wa tarakilishi yaani, kinga virusi.
4. Kutoa fursa ya utunzaji wa data au taarifa katika maeneo tofauti ili kuhakikisha usalama wa data.
5.Kurahisisha mawasiliano. Mfano, matumizi ya baruapepe katika ofisi. biashara, elimu na sehemu zote za kutolea huduma
6.Kupunguza gharama za ununuzi wa karatasi, uchapaji na usafiri wakati taarifa zinatumwa kwa mtandao.
7.Kuongeza ufanisi katika utendaji wa mtu binafsi au taasisi
Aina za mtandao
Mtandao unaweza kuainishwa kulingana na ukubwa wa eneo la kijiografia ambalo andao huo unatumika. Utajifunza aina kuu mbili za mtandao zinazojulikana zadi ambazo ni Mtandao Janibu (MJA) na Mtandao Mpana (MTΑΡΑ).
Mtandao Janibu (MJA): Aina hii ya mtandao huunganisha tarakilishi ndani ya aneo dogo la kijiografia kama vile chumba cha ofisi, jengo, shule, makazi Jumaabara. Mara nyingi mtandao huu hutumia nyaya kuunganisha vitumi yake. Pla, unaweza kuunganisha vitumi mbalimbali kwenye mtandao bila utumia waya. Mtandao Janibu unaweza kumilikiwa na mtu binafsi, shule, kampuni au shirika. Matumizi ya mtandao huu ni kwa ajili ya watu wa eneo husika mfano, wafanyakazi wa kampuni au shirika, jumuiya ya shule au chuo.

Faida za matumizi ya Mtandao Janibu (MJA)
1. Ufungaji na uunganishaji wake hauhitaji gharama kubwa sana.
2. Ni rahisi kuusimamia na kuuendesha kwa kuwa upo eneo moja.
3. Vitumi vyake hupatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu.
4. Mtandao huu ni rahisi kushirikishana faili kwa ufanisi mkubwa.
5. Ni rahisi kuanzisha utaratibu wa usalama ili kulinda utumiaji wa mtandao
6. Hutoa nafasi ya kuhifadhi machapisho kwa matumizi ya pamoja. Mfano kwa kutumia seva.
7. Programu tumizi na endeshi vinaweza kutumika kwa ushirikiano bila kulazimika kununua nyingi.
Hasara za kutumia Mtandao Janibu
1. Hutoa mawasiliano katika eneo dogo la kijiografia.
2. Ni rahisi kuzifikia programu za ndani ya mfumo na kuhatarisha usalama wa taarifa za watumiaji.
3. Seva ikipata madhara, watumiaji wote huathirika.
4. Ni rahisi virusi vya tarakilishi kusambaa ndani ya mtandao.
5. Unahitaji wataalamu wenye ujuzi ili kuuanzisha, kuudhibiti na kuuendesha
Mtandao Mpana (MTAPA): Kampuni au taasisi zinapoanzishwa huanza na tawi moja. Tawi hujengewa mtandao wake wa ndani kwa ajili ya shughuli zake na mawasiliano kulingana na eneo. Baada ya muda kampuni hukua na kupanua shughuli zake nje ya eneo lake. Kwa mfano, kutoka mji mmoja kwenda mwingine au kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Pia, kutoka ndani na nje ya nchi. Kila tawi linalofunguliwa hujengewa Mtandao Janibu. Iwapo matawi haya yataunganishwa na makao makuu yake ili kupeana taarifa. data na kufuatilia utendaji wa pamoja, mtandao utakaoundwa utaitwa Mtandao Mpana. Kwa hiyo, Mtandao Mpana ni mtandao unaochukua eneo kubwa la kijiografia kama vile nchi, bara hata dunia.

Faida za kutumia MTAPA
1. Hutoa mawasiliano katika eneo kubwa la kijiografia.
2. Huruhusu kutumia rasilimali na programu tendaji kwa pamoja kutokea sehemu mbalimbali.
3. Hutoa nafasi ya kuingia na kutumia masoko ya biashara za kitaifa ra kimataifa.
4. Husaidia mawasiliano ya haraka kwa wote walio katika mtandao huu katika nchi au duniani kote.
Hasara za kutumia MTAΡΑ
1. Usalama wake ni mdogo ukilinganisha na Mtandao Janibu.
2. Gharama za kufunga na kuunganisha ni kubwa sana.
3. Gharama za uendeshaji ni kubwa.
4. Unahitaji matumizi ya programu ya kuzuia udukuzi wa data na taarifa
0 Comments: