NGELI ZA NOMINO
NGELI ZA NOMINO:Ni makundi ya kisarufi ya majina katika lugha ya kiswahili na baadhi ya lugha za kibantu.Kwa maneno mengine, ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika makundi yanayofanana kwa kuzingatia umoja na uwingi wa maneno hayo.silabi zilizokolezwa wino ndio zinazounda aina ya ngeli.
Ngeli hizo zipo za namna tisa ambazo zimeainishwa kama ifuatavyo:
1.Ngeli ya A-WA
Ngeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile watu,wanyama,ndege,wadudu nk.
Umoja uwingi
Mfano:Msafiri anakaribia kufika. Wasafiri wanakaribia kufika
2.Ngeli ya U-I
Ngeli hii inahusisha majina ya vitu visivyohai vinavyoanza na sauti M (umoja)na ya(uwingi) pia baadhi ya viungo vya mwili huingia hapa mfano mguu,mkono,mkia nk.
Umoja uwingi
Mfano:Mtiunaungua moto Miti inaungua moto
3.Ngeli ya LI-YA
Ngeli hii hujumuisha majina yenye kiambishi awali(umoja)na ya (uwingi)
Umoja uwingi
Mfano:Chungwa limeiva. Machungwa yameiva
4.Ngeli ya KI-VI
Hii ni ngeli ambayo hujumuisha majina yanayoanza na ki au ch(umoja) na vi au vy(uwingi)
Umoja uwingi
Mfano:Kitandakimetandikwa Vitanda vimetandikwa
Chakulakitaliwa Vyakula vitaliwa
5.Ngeli ya U-ZI
Ngeli hii hurejelea majina ambayo huanza na U katika umoja na kuchukua ZI kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika uwingi.
Umoja uwingi
Mfano:Ufaumejitokeza Nyufa zimejitokeza
Ukuta umejengwa Kuta zimejengwa
Wimbo unachezeka Nyimbo zinachezeka
6.Ngeli ya I-ZI
Ngeli hii hutumika kwa majina yasiyobadilika katika umoja wala katika uwingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: i (umoja) na zi (uwingi)
Umoja uwingi
Mfano:Nyumba imebomoka Nyumba zimebomoka
7.Ngeli ya U-YA
Ngeli hii hujumuisha nomino zenye kiambishi awali U(umoja) na ma(uwingi)
Umoja uwingi
Mfano:Unyoya unapepea Manyoya yanapepea
8.Ngeli ya KU
Katika ngeli hii yanaingia majina yote yanayotokana na kunominisha vitenzi
Mfano:Kuimba kumemtajirisha
Kutembea kumemchosha
9.Ngeli ya PAMUKU
Ngeli hii huonesha mahali
Mfano: Hapa petu pazuri Mfano:
Mfano: Pale palipo na upendo Mfano: Mule mulimoungua
0 Comments: