OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA RUVUMA
HALMASAURI YA WILAYA YA TUNDURU
UPIMAJI WA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI …………………………OKTOBA 2025
SOMO: JIOGRAFIA NA MAZINGIRA, SANAA NA MICHEZO
JINA LA MWANAFUNZI........................................................
MUDA: SAA 1:30
Maelekezo
1. Karatasi hii ina maswali Matano (5)
2. Jibu maswali yote kwenye nafasi uliyopewa ukifuata maelekezo ya kila swali.
1. Andika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano.
- Michoro midogo inayotumika kwenye ramani kuwakilisha vitu halisi huitwa ______________ (A) Alama za ramani (B) vipengele vya ramani (C) ufunguo (D) michoro ( )
- Taka za plastiki zisipohifadhiwa vizuri zinaharibu mazingira kwa sababu ____________ (A) Zinachukua nafasi kubwa (B) zinatoa harufu (C) zinachukua muda mwingi kuoza ( )
(D) zinaweza kulipuka
- Ni aina gani ya ramani huonesha maumbo ya asili na yaliyotengenezwa na binadamu? (A) Ramani za kisiasa (B) ramani za topografia
(C) ramani za thematiki (D) ramani za jumla ( )
- Mwalimu wa jiografia na mazingira alikuwa anawafundisha wanafunzi wa darasa la tatu kuhusu faida za kilimo. Ipi kati ya zifuatazo siyo faida ya kilimo? ( )
(A) Kupata chakula (B) kupata malighafi zinazotumika kiwandani
(C) chanzo cha fedha (D) kivutio cha utalii
- Ipi kati ya zifuatazo ni Sanaa za maonesho?
(A) Majigambo (B) maigizo (C) maleba (D) hadithi ( )
2. Oanisha fungu A na fungu B ili kupata maana sahihi.
NA | Fungu "A" | MAJIBU | Fungu "B" |
i | Kayamba, manyanga na njuga | | 1. Maleba 2. Ala za kutikisa 3. Hadhira 4. Sauti kateka uigizaji 5. Igizo 6. Kisigino kidoleni na hatua za mzabibu |
ii | Onesho linalofanyika wakati wa kuigiza | | |
iii | Mazoezi ya kujisawazisha na kuufanya mwili kuwa mwepesi | | |
iv | Mtu anayeangalia Sanaa za maonesho | | |
v | Mavazi yanayovaliwa wakati wa uigizaji | |
- ______________________ ni mchoro unaowakilisha taarifa zilizopo katika uso wa dunia kwa kutumia skeli maalumu
- Ramani zinazotoa taarifa kuhusu mipaka ya nchi , mikoa, wilaya na maeneo mengine ndani ya nchi ________________________________________________________________________
- ____________________ ni umbo la ardhi lenye mwinuko mrefu Zaidi juu ya uso wa dunia.
- Mpaka au mstari wa nje unaozunguka ramani huitwa ________________________________
- Maliasili zinazopatikana ardhini _________________________________________________
4. Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata:
Ufugaji ni shughuli inayohusu kutunza mifugo kama vile ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku na bata. Kuna aina tatu za ufugaji, miongoni mwa aina hizo za ufugaji ni ufugaji wa kuhama hama. Nchini Tanzania ufugaji wa kuhamahama hufanywa na makabila matatu: wasukuma, wamasai na wabarabaig. Wafugaji huhama hama kwa ajili ya kutafuta malisho na maji. Ufugaji huu husababisha uharibifu wa mazingira kama vile mmomonyoko wa udongo, ukataji miti ovyo na kuondolewa kwa uoto wa asili. Uharibifu huu wa mazingira unaweza kudhibitiwa kwa kutoa Elimu kwa wafugaji kwa kuwapa mbinu bora za ufugaji.
Maswali
- Shughuli inayohusu utunzaji wa mifugo huitwa _______________________________________
- Taja makabila matatu yanayojihusisha na ufugaji wa kuhama hama nchini Tanzania: _________________________ , ________________________ , _________________________
- Kuna aina ngapi za ufugaji zilizotajwa katika habari uliyosoma? __________________________
- Taja sababu mbili zinazofanya wafugaji kuhama hama kutoka sehemu moja kwenda nyingine
1. ____________________________________________________________________
2. ____________________________________________________________________
3. ____________________________________________________________________
- Ni njia gani iliyotajwa ili kudhibiti madhara yatokanayo na ufugaji wa kuhamahama?_______________________________________________________________
5. Chunguza kielelezo kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata hapo chini.
- Ni upande gani wa dunia unawakilishwa na namba 1? __________________________________
- Ni upande gani wa dunia unawakilishwa na namba 2? __________________________________
- Ni upande gani wa dunia unawakilishwa na namba 3? __________________________________
- Namba 4 inawakilisha upande gani wa dunia? ________________________________________
- Namba 5 inawakilisha upande gani wa dunia? ________________________________________
MAJIBU
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA drs iv
Swali la 1
- A
- C
- B
- D
- B
Swali la 2
- B
- E
- F
- C
- A
Swali la 3
- Ramani
- Ramani za kisiasa
- Mlima
- Fremu
- Madini
Swali la 4
- Ufugaji
- Wasukuma, wamasai na wabarabaig
- Tatu
- Malisho na maji
- Kutoa elimu kwa wafugaji
Swali la 5
- A Kas – Mas
- B Kus – Mas
- C Kus – Magh
- D Magh
- E Kas - Magh
Imeandaliwa na:
nampunguprimaryschool
0 Comments: