Sunday, March 08, 2026

Jinsi ya kufundisha mada inayohusu hesabu za seti
*SETI* 
 *DHANA YA SETI*
Katika hisabati na katika maisha ya ila siku tunazungumza juu ya mkusanyiko wa vitu, wanyama, watu n.k
Kwa hiyo maana ya SETI ni mkusanyiko maalumu wa vitu.

 *MEMBA WA SETI*
-Ni vitu vilivyomo katika SETI.
Seti huitwa kwa herufi kubwa na tunatumia mabano maalumu. {  } au (Curl blackest)
Mfano:Seti ya namba nzima ndogo kuliko 6
      N={0,1,3,4,5}
Alama ya memba ni €.
Kwa kutumia mfano wa hapo juu 0€N,1€N,2€N,3€N,4€N,5€N
Kama sio memba wa Seti ni €/
Mfano 6€N,7€8




 *Njia za kueleza Seti* 
(i) Njia ya Maelezo
Ni seti ambayo inaelezwa kwa njia ya Maelezo.
Mfano:Seti ya namba nzima ndogo kuliko 6

(i) Njia ya kuorodhesha au kutaja namba za Seti.
Mfano:   A={7,9,11,13}
Seti A ni seti ya namba nzima kubwa kuliko 6 na ndogo kuliko 14 au *6>7,9,11,13<14* 

 *AINA ZA SETI* 
(1) *_SETI TUPU_* 
Ni seti yoyote ambayo haina memba na inaoneshwa kwa alama {  }  au °0°

(2) *_SETI SAWA_*
Ni seti zenye memba walewale isipokuwa hutofautiana kwenye nafasi zake
Mfano: A={a,b,c,d}
             B={c,a,d,b}

(3) *_SETI ZINAZOLINGANA_*
Ni seti ambazo idadi ya memba wa Seti zote mbili ni sawa ingawa memba ni tofauti
Mfano: A={a,b,c}
             B={2,3,4}
(4) *_SABSETI(Alama ya sabseti ni C)_*
Mfano:  A={a,b,c,d,e}
              B ={a,b,c,e}
              C={a,b}
              D={e}
Memba wa Seti B,C na D hupatikana kwenye seti A
Hivyo basi BCA,CCA na DCA au BCDCA

(5) *_SETI KUU(Alama ya seti kuu ni U)_* 
Kwa kutumia seti za namba nne
            A={}
Seti A ni seti kuu ya seti B,C,D au AUB,C,D

 *MATENDO KATIKA SETI* 
 _(i)Muungano U (union)_ 
 _(ii)Ungano(Intersection)_ 
 _(iii)Kikamilisho(Compliment)_ 

 *I: _MUUNGANO (U) WA SETI_* 
Tunaweza kuunganisha seti mbili kupata seti moja.
         A={1,3,5,7,9}
         B={0,2,4,6,8}
AUB={0,1,2,3,4,5,6,7,8,9}

 *_II: UNGANO (n) LA SETI_* 
Tunaweza kuonyesha Ungano la seti mbili kwa kutumia michoro ya Venn
                            A={1,2,3,4,5,6}
                            B={4,5,6,7,8,9}



                                *AnB={4,5,6}* 

 *KIKAMILISHO CHA SETI* 
Fikilia Seti zifuatazo
 U={0,1,2,3,4,5,6,7, 8,9}
 B={6,7,8,9}
Katika mchoro wa Venn



Kwa hiyo Kikamilisho cha seti B ni 0,1,2,3,4,5
Alama ya Kikamilisho cha seti A ni A' na husomwa A Chali
                         *_Yaani A'={0,1,2,3,4,5}_* 

 *IDADI YA MEMBA KATIKA SETI* 
Angalia seti zifuatazo
                A={1,2,3,4,5,6}
                B={a,b,c,d,e,f,g}
                C={Embe,Chungwa,Nyanya}
                D={Seti ya herufi zote za alfabeti}

Tabia ya idadi ya memba katika seti
(i)Iwapo seti kuu ni seti yenye kikomo na seti A ni sabseti yake.
                          *_Basi n(A)=n(U)-n(A)_*
(ii) Iwapo A na B ni seti zenye kikomo basi
              *_*n(AUB)= n(A)+n(B)-n(AUB)_** 

 *IDADI YA SABSETI KATIKA SETI* 
Kanuni 2 kipeuo cha n.n ni idadi ya subset
 *Mfano* E={a,b}
Seti hii 🖕ina subset 2 yaani E={a},E={b}
Kwa hiyo itakuwa
                              2x2=4
Hiyo idadi ya subset ni 4
           *_{ },{a},{b},{a,b}_**

Imeandaliwa na Testme:
   

Wednesday, February 25, 2026