Huduma za afya ni mahitaji mbalimbali yanayotolewa kwa jamii ili kujenga afya. Miongoni mwa huduma hizo ni elimu ya uzazi wa mpango na utoaji dawa kwa waathirika wa vvu na ukimwi.
Uzazi wa mpango ni nini?
Uzazi wa mpango ni utaratibu wa kupata watoto unaotokana na makubaliano kati ya mke na mume juu ya idadi ya watoto na muda wa kuwapata kwa kuzingatia afya ya mke na uwezo wa kuwatunza.
Njia za uzazi wa mpango
Kuna njia mbalimbali za uzazi wa mpango ambazo mke na mume wanaweza kukubaliana kuzitumia. Njia hizo ni kama vile
1.Njia za asili za uzazi wa mpango
Ni njia ambazo zinazuia mke kupata mimba bila kutumia dawa au vifaa maalumu. Zifuatazo ni baadhi ya njia za asili:
(i) kutojamiiana wakati wa kupindi cha hatari
Mzunguko mmoja wa hedhi huwa siku 28 kwa baadhi ya wanawake tangu hedhi ya moja hadi nyingine
(ii) Kutomwaga gametiume kwenye uke wakati wa kujamiiana
(iii) Mama kuendelea kumnyonyesha mtoto ipasavyo. Anapomnyonyesha mtoto ipasavyo hedhi hukoma mpaka atakapomwachisha kunyonya
2.Njia za kisasa za uzazi wa mpango
Ni njia ambazo hujumuisha matumizi ya vifaa na dawa.vifaa hivyo ni kama vile
(i) kondomu: kondomu huvaliwa na mwanaume au mwanamke wakati wa tendo la kujamiiana.hivyo manii hayaingii ukeni
Faida za kutumia kondomu
- Huzuia mimba na baadhi ya magonjwa ya zinaa
- Haihitaji kwenda kumuona daktari
- Hupatikana kwa urahisi
Huhamasisha ukahaba na umalaya
(ii) Kiwambo: kiwambo huwekwa ndani ya uke kwenye seviksi ili kuzuia manii kuingia
Faida za kutumia kiwambo
- Huzuia kansa ya shingo ya kizazi kwa kiasi FulaniMadhara ya kutumia kiwambo
- Kinaweza kuwekwa vibaya na kuruhusu mimba kutunga
Faida za kutumia kitanzi
- Kikishawekwa hakuna haja ya kufanya kitu chochote cha ziada
- Kina uhakika mkubwa wa kuzuia mimba
- Huweza kusababisha maumivu na damu nyingi wakati wa hedhi
- Huweza kuleta maambukizi katika kizazi yanayoweza kuleta utasa
- Kama mimba ikitokea inaweza kuwa kwenye mirija ya falopio
Faida za kutumia Vidonge
- Ni rahisi kutumia, huzuia mimba na huweza kuzuia baadhi ya uvimbe
- Huweza kusababisha aina fulani ya uvimbe, shinikizo la damu na damu kuganda
- Ni rahisi kusahau kumeza Vidonge
- Vinahitaji kutumiwa kila siku
Faida za Kukata mirija ya manii na falopio
- Ina uhakika wa 100% wa kuzuia mimba
Madhara ya Kukata mirija ya manii na falopio
- Si rahisi kuja kuunganisha tena mirija ya manii na falopio kama watataka kuzaa tena
FAIDA ZA UZAZI WA MPANGO
1.kujenga afya
2.upatikanaji wa mahitaji
3.Mafanikio ya kiuchumi
4.kuepuka maradhi
5.kuwa na amani na upendo
MADHARA YA KUTOPANGA UZAZI
1.kuwa na afya dunia
2.kukosa mahitaji ya msingi
3.kuwa na umaskini
4.kukumbwa na maradhi mbalimbali
5.kukosa amani na upendo ndani ya familia
0 Comments: