Saturday, November 9, 2024

**Ukimwi (UKIMWI)** ni kifupisho cha "Upungufu wa Kinga Mwilini" na ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya HIV (Human Immunodeficiency Virus). Virusi hivi hushambulia mfumo wa kinga ya mwili, na kuufanya mwili kushindwa kupambana na maambukizi na magonjwa mbalimbali¹.

**Njia za Maambukizi ya HIV:**
- Kufanya ngono bila kinga.
- Kuchangia sindano.
- Mama aliyeambukizwa anaweza kumwambukiza mwanawe wakati wa uja uzito, kuzaa au kunyonyesha.
- Kutangamana kwa damu au majimaji mengine ya mwili².

**Dalili za Ukimwi:**
- Kupungua uzito bila sababu.
- Homa za mara kwa mara.
- Uchovu usioelezeka.
- Kuumwa na koo na vidonda vya mdomo.
- Maambukizi ya mara kwa mara².

**Kinga na Tiba:**
- Hakuna tiba ya kuponya Ukimwi, lakini kuna dawa za kupunguza makali ya virusi (ARVs) ambazo husaidia wagonjwa kuishi maisha marefu na yenye afya zaidi.
- Kujikinga ni pamoja na kutumia kondomu, kuepuka kuchangia sindano, na kupima afya mara kwa mara².

**Madhara ya Ukimwi:**
- Husababisha vifo vya watu wengi, hasa barani Afrika.
- Huathiri uchumi na jamii kwa ujumla kutokana na kupoteza nguvu kazi¹.

Mambo ya kuzingatia kwa waathirika wanaotumia “ARV”
Waathirika wa VVU ni kundi linalohitaji kuishi kwa kufuata taratibu
zilizoainishwa na wataalamu wa afya. Mambo ya kuzingatia ni kama
yafuatayo:
1. Waathirika ni lazima wafuate ushauri wa kitaalamu wa kitabibu au
wataalamu wa afya.
2. Waathirika wanapaswa kutumia “ARV” kwa dozi sahihi na kwa muda
sahihi. Dawa zitumike kama ilivyoelekezwa na daktari au mtaalamuwa afya. Hii itasaidia kuboresha afya na kupunguza uwezekano wa

VVU kuwa sugu kwa dawa zinazotumika.
3. Waathirika wachukue tahadhari kwa kujikinga ili wasipate
maambukizi mapya na kuambukiza wengine.
4. Mwathirika asiache kutumia dawa kwa muda na kisha kurudia tena
dawa hizo bila ushauri wa daktari au mtaalamu wa afya.
5. Waathirika wa VVU watoe taarifa kwa daktari au watoa huduma
kuhusu matatizo na athari za “ARV” endapo zitajitokeza.
6. Waathirika waepuke kufuata imani na mila potofu za jadi au za dini
zinazozuia kuwa mfuasi mzuri wa “ARV”.
7. Waathirika wafuate ratiba ya kwenda kliniki ya dawa za “ARV” bila
kukosa.
8. Waathirika wazingatie kanuni za afya kwa mfano, kuzingatia usafi
wa mwili, lishe bora na mazingira safi.
9. Waathirika wanashauriwa kuendelea kuishi kwa matumaini na
wasikate tamaa.
10. Mtumiaji wa “ARV” haruhusiwi kushirikiana dawa zake za “ARV” na Kujali watu wanaotumia dawa za “ARV”
Waathirika wa VVU wanaotumia “ARV” wanahitaji kuthaminiwa na jamii.
Ili kuwajali watu wanaotumia dawa za “ARV” ni muhimu sana kuwasaidia
pale wanapohitaji msaada.

Tunaweza kuwajali kwa kufanya yafuatayo:
1. Kuambatana nao wanapohitaji kusindikizwa kwenda kliniki kuchukua
2. Tuwasaidie wanapohitaji kuelekezwa matumizi sahihi ya “ARV”.
3. Kuwapatia chakula bora na kwa wakati.
4. Kuwakumbusha muda sahihi wa kumeza dawa pale wanaposahau.
5. Kuwahamasisha kuendelea na matumizi ya dawa.
6. Kuepuka kuwanyanyapaa walioathirika na VVU.
Umuhimu wa ushauri unaotolewa na daktari kwa watumiaji
wa “ARV”
Ni muhimu sana kuzingatia na kufuata ushauri unaotolewa na daktari au
mtaalamu wa afya kwa mtumiaji wa “ARV”. Ushauri wa daktari unamsaidia
mtumiaji wa “ARV” aweze kufanya yafuatayo:
1. Kutumia dawa kwa kipimo na wakati sahihi.
2. Kuelewa maendeleo ya afya yake.
3. Kuepuka kufuata mila potofu zinazozuia kuwa mfuasi mzuri wa
“ARV”.
4. Kuboresha afya na kupunguza uwezekano wa VVU kuwa sugu kwa
dawa anazotumia.
5. Kutokata tamaa.
Sehemu A: Chagua jibu sahihi katika maswali haya.

0 Comments:

Advertisement