Thursday, August 14, 2025

WALIMU NA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI


*๐Ÿ–ฅ️ WALIMU NA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI*

Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inaendana na mabadiliko ya dunia ya sasa, 

*Serikali kupitia Wizara ya Elimu* imeweka mkazo mkubwa juu ya *matumizi ya TEHAMA mashuleni*, hasa katika utekelezaji wa *mtaala ulioboreshwa*.

๐ŸŽฏ *Lengo kuu:*  
Kuhakikisha *kila mwalimu* anakuwa na uelewa na ujuzi wa msingi wa TEHAMA katika kufundisha na kujifunza. Hili ni *hitaji rasmi* siyo hiari tena.
Published from Blogger Prime Android App

✅ UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO HAYA

Walimu waliowahi kupata mafunzo rasmi ya TEHAMA wameelekezwa kwenda *kuwajengea uwezo walimu wenzao mashuleni* kwa njia ya mafunzo kwa vitendo. Hili ni agizo la serikali – kila shule ihakikishe inatenga muda wa ndani ya wiki kwa ajili ya mafunzo hayo ya ndani.

Hivyo basi Wasimamizi wa ELIMU Ngazi ya Shule, Kata , Halmashauli na Mkoa Wanapaswa Kuhakikisha walimu wao wanawezeshewa Elimu Hii.

๐Ÿง  MAMBO MUHIMU AMBAYO WALIMU WANAPASWA KUPEANA UJUZI KWA PAMOJA NI PAMOJA NA HAYA YAFUATAYO.

1. *Uelewa wa mtaala mpya na nafasi ya TEHAMA*  

   Mtaala mpya umeainisha wazi kuwa matumizi ya TEHAMA ni sehemu ya lazima ya ufundishaji. 

Hakuna mwalimu atakayekwepa matumizi ya TEHAMA katika somo lolote. Hivyo Kila shule ihakikishe inafanya kazi Hiyo.

2. *Kutambua vifaa vya TEHAMA vinavyotumika mashuleni*. Walimu wafahamu matumizi ya vifaa kama vile :  

   - Kompyuta (desktop au laptop)  
   - Simu janja  
   - Tablet  
   - Projector  
   - Printer  
   - Smart board  
   - Spika, kamera, microphone n.k.

3. *Matumizi ya Artificial Intelligence (AI) mfano Chatgpt*  

   Tanzania imeandaa mwongozo rasmi wa matumizi ya AI katika elimu. 

Walimu wanapaswa kufahamu namna ya kutumia AI kama nyenzo ya kuongeza ubunifu na ufanisi katika ujifunzaji na ufundishaji.

4. *Ujuzi wa Microsoft Office*  
   - *Word* kwa maandalizi ya nyaraka  

   - *Excel* kwa taarifa za wanafunzi na ripoti mbalimbali  

   - Hii ni muhimu sana katika kazi za kiutawala na kitaaluma.

5. *Matumizi ya majukwaa ya kidigitali:*  
   - Zoom, Email, WhatsApp, Google Forms, Telegram, YouTube n.k.  

   - Walimu wafundishane namna ya *kujisajili, kuunda, na kutumia* majukwaa hayo kwa kufundishia.

6. *Uunganishaji wa vifaa (Connectivity Skills)*  
   - Kufahamu jinsi ya kuunganisha vifaa kwa *cables* au *wireless* 

   - Hii ni pamoja na kufahamu mifumo ya projector, smart boards, na vifaa vinavyosaidia kazi za kitaaluma.

๐Ÿ—“️ RATIBA YA UTOAJI UJUZI SHULENI
Kila shule inapendekezwa *kutenga muda maalum kila wiki* (kwa mfano mara 2 Hadi mara 4 ) kwa walimu *kukutana na kushirikishana ujuzi wa TEHAMA*. 

Hili sio hiari, ni *agizo rasmi la serikali* na linaenda sambamba na utekelezaji wa mtaala mpya.

๐ŸŽฅ MAFUNZO HAYA PIA YANAPATIKANA KWA NJIA YA MTANDAONI

Ili kuendelea kujifunza, fuatilia *mafunzo,  kipengele kwa kipengele* kupitia majukwaa yafuatayo ya *ElimikaLeo

๐Ÿ“ฒ *WhatsApp Channel:*  

๐Ÿ“˜ *Facebook:*  
๐Ÿ‘‰ https://www.facebook.com/profile.php?id=61574011348247

▶️ *YouTube:*  
๐Ÿ‘‰ https://youtube.com/@ElimikaLeo

๐Ÿ“ฑ*Instagram:*                         
๐Ÿ‘‰https://www.instagram.com/@elimikaleo_tz  
 
๐Ÿ“ฑ*Telegram channel:*   
  ๐Ÿ‘‰ https://t.me/ElimikaLeo 

๐ŸŒ*Website*
๐Ÿ‘‰ msomihurutzblog.blogspot.com
                    
*๐Ÿ—ฃ️ USISITE KUSHARE NA WALIMU WENZAKO*  
Elimu ya TEHAMA ni jukumu la kila mmoja wetu   tusaidiane kufanikisha lengo hili la kitaifa!

By
ElimikaLeo

0 Comments:

Advertisement