VIPIMO VYA METRIKI YA UREFU,UZANI NA UJAZO
Vizio vya metriki vya Urefu
META(M)
Kipimo cha msingi cha meta katika vipimo vya metriki ni Meta.
Meta hutumika kupima Urefu na upana na vitu kama nguo za kuvaa,vitanda,madawati n.k
SENTIMETA(SM)
Kikubwa kwenda kidogo UNAZIDISHA
Kidogo kwenda kikubwa UNAGAWANYA
Zana
RULA
>Kwa kawaida RULA inaurefu wa SM 30.Ndani ya kipimo hiki kila sm1 huonyesha visehemu vidogovidogo ambayo kila kimoja ni Mm.
Hivyo RULA ni Sm 30=Mm 300
Kipande cha RULA
JEDWALI LA KUONESHA UHUSIANO WA VIPIMO VYA METRIKI VYA UREFU
Km Hm Dam M Dm Sm Mm
1 0 0 0 0 0 0
1 0 0 0 0 0
1 0 0 0 0
1 0 0 0
1 0 0
1 0
NJIA YA KUFUNDISHIA VIPIMO VYA UREFU
Uhusiano Kati ya Vizio na jinsi utakavyo mfundisha mwanafunzi.
Mfano
Km 1 ina M ngapi?
Hatua ya kwanza
Mwalimu amwongoze mwanafunzi afahamu vizio kwa kutengeneza jedwali linaloeleza uhusiano wa Vizio.
Hatua ya Pili
Mwalimu amwongoze mwanafunzi kuweka kalamu kwenye safu ya Km.
Hatua ya tatu
Mwalimu amwongoze mwanafunzi kuteremsha kalamu hadi 1 yaani Km 1
Hatua ya nne
Mwanafunzi aelekeze kalamu kwenye mstari huo hadi kwenye safu ya M ukute M 1000
Hatua ya tano
Mwanafunzi aandike jibu 1000 au aseme au aandike
UZANI
Dhana ya UZANI ni upimaji wa uzito wa vitu kwa kutumia zana ya Mizani
Kwa hiyo Mizani hupimwa kwa kutumia vizio vya uzito.
Vizio vya uzito katika metriki ni kama ifuatavyo;
Kipimo cha msingi ni Gramu(g).Gramu hutumika kupima vitu vidogovidogo kama vile madawa, viungo vya wanyama,sukari n.k
JEDWALI LA KUONESHA UHUSIANO WA VIPIMO VYA METRIKI VYA UZANI
Kg Hg Dg G dg Sg Mg
1 0 0 0 0 0 0
1 0 0 0 0 0
1 0 0 0 0
1 0 0 0
1 0 0
1 0
Vizio vya uzito vinapishana kwa ngazi za kumi kumi
Vizio vya juu ni Dg ambacho ni ni mara 10 ya Gramu
Hg ni mara 100 ya Gramu
Kg ni mara 1000 ya Gramu
VIPIMO VYA CHINI
dg ambacho ni ¹/10 ya Gramu
Sg ambacho ni ¹/100 ya Gramu
Mg ambacho ni ¹/1000 ya Gramu
UJAZO
Maana
Tunapozungumzia ujazo tunamaana kuwa ni kiasi cha kitu kilichomo ndani ya chombo Au Ni kiasi cha nafasi iliyo ndani ya chombo
Vizio vya ujazo vya metriki katika vipimo vya metriki
Kipimo cha msingi cha UJAZO ni Lita
JEDWALI LA KUONESHA UHUSIANO WA VIPIMO VYA METRIKI VYA UJAZO
KL HL DL L dL SL ML
1 0 0 0 0 0 0
1 0 0 0 0 0
1 0 0 0 0
1 0 0 0
1 0 0
1 0
Vipimo vya ujazo ambavyo hutumika mara nyingi ni military(ml)
Vizio vya metriki vya ujazo vinaweza kufupishwa
0 Comments: