Saturday, January 17, 2026

Ukitaka kuheshimiwa na kuwa na kibali iwe mkubwa au mdogo fanya yafuatayo


Ukitaka kuheshimiwa na kuwa na kibali fanya yafuatayo



A. Muweke Mungu mbele katika Kila Kitu yeye atakutambulisha kwa watu kwa wakati wake. 

B.  kuwa mnyenyekevu hata Kama itakugharimu najua sio kitu rahisi ila Mungu atakuwezesha. 

B. Usijitambulishe kwa watu Kama hakuna ulazima.  Yaani Elimu, Cheo au vyovyote kama hawajakuuliza. 

C. Usimwambie kila anayekuzunguka uhitaji wako Kama hakuna ulazima. 
Yaan pigana mpaka dakika ya mwisho ikishindikana ndipo ufanye hivyo na sio unaanza jambo na wazo la kuomba msaada kabla ya kupambana. 

D. Ishi kwa Imani yaani ona yote yanawezekana. 

E. Unapokuwa umekosea omba msamaha Kwa lengo la kuhuzunika kukosea na kukusudia kutorudia Kosa . Sio kuomba msamaha Ili yaishe. 

F. Heshimu mipango na maono ya watu wengine na kuwaombea wafanikishe. 
G.  Usitoe siri zako za ndani Sana Kama hakuna ulazima.

E.  Usitangaze jambo kubwa la kibinafsi unalotarajia kulifanya  siku kadhaa zijazo hata Kama una imani Kubwa ya kulifanikisha Kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo

F. Usifanye chochote na usiseme chochote popote, wakati wowote yaani kila kitu na Muda na mahali pale.
KUMBUKA
heshima huvuta kibali. 

Usitumie nguvu kubwa kutafuta heshima wala hauhitaji mabango makubwa Bali endelea kujifunza.  Pointi zitaendelea.

0 Comments: